Home Kitaifa Kotei ametaja viungo 6 wazawa wanaomfanya awatazame

Kotei ametaja viungo 6 wazawa wanaomfanya awatazame

18930
0
SHARE

Kiungo mkabaji wa Simba Mghana James Kotei kupitia ukurasa wake wa Instagram (james_kotei) ameorodhesha viungo wazawa anaowakubali kwenye ligi kuu Tanzania bara (VPL).

Katika orodha hiyo ya viungo sita (6) wazalendo wapo Said Ndemla (Simba), Mwinyi Kazimoto (Simba), Shabani Kisiga (Ruvu Shooting), Himid Mao ‘Ninja’ (Azam FC), Abubakar Salum ‘Sure Boy’ (Azam FC) na Hassan Dilunga (JKT Ruvu).

Kotei ambaye wakati mwingine hupangwa kama beki wa kati wa Simba hajamtaja alijiunga na Simba wakati wa dirisha dogo la usajili na amekuwa nguzo muhimu ndani Wekundu wa Msimbazi tangu alipoanza kupewa nafasi mara kwa mara kwenye michuano ya Mapinduzi Cup mapema mwaka huu.

Raia huyo wa Ghana amejihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kochs Joseph Omog na amecheza mechi nyingi za ligi pamoja na michuano ya FA Cup (ASFC) ukulinganisha na baadhi ya wachezaji ambao aliwakuta kwenye kikosi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here