Home Kitaifa Kisiga ameipa Simba ubingwa

Kisiga ameipa Simba ubingwa

11444
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

KIUNGO wa Ruvu Shooting, Shaban Kisiga amesema kwamba Simba ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa endapo watakuwa makini na kuwatumia vizuri wachezaji wao ambao wengi ni vijana wapambanaji kuliko Yanga ambayo inatumia uzoefu zaidi.

Kisiga ambaye aliwahi kuichezea Simba miaka ya nyuma akizungumza na Shaffihdauda.co.tz alisema kuwa jambo pekee la kujivunia kwa Simba ni kuwa na vijana wa aina hiyo wenye uwezo wa kucheza pasipo kuchoka kutokana na umri wao mdogo.

“Simba ina vijana wengi wenye vipaji, hawachoki kupambana ukilinganisha na Yanga ambao wanatumia uzoefu sana kuusaka ubingwa, Yanga kwa uzoefu wao na kama watatwaa ubingwa ni kwa vile kila mchezaji anaonekana kuwa kiongozi kwa mwenzake, hivyo wanaweza kutumia uzoefu wao,” alisema Kisiga.

Hata hivyo, Kisiga alisema kuwa ingawa Simba wana nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa bado wanahitaji kupambana zaidi kwa kuongeza juhudi pamoja na umoja ili kufikia malengo kwani hata Yanga wana nia ya kutetea ubingwa wao.

Simba ndiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 55 huku Yanga wakishika nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 53 na timu zote zimecheza mechi 24 kila moja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here