Home Kitaifa Yanga wameamua kufata nyayo za Simba

Yanga wameamua kufata nyayo za Simba

5136
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

UONGOZI wa klabu Yanga umekubali mwaliko kutoka chama cha soka mkoani Dodoma (DOREFA) kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Polisi Dodoma Machi 25.

Mwaliko huo unakuja wiki moja baada ya watani wao Simba kufanya ziara mkoani humo na kucheza na Maafande hao waliowafunga mabao 3-0.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Boniface Mkwasa uongozi umekubali mwaliko huo ambapo Machi 25 watashuka katika uwanja wa Jamhuri mkoani humo tayari kwa mchezo huo wa kirafiki.

Chama hicho kiliandika barua Machi 14 kwa Yanga ambapo uongozi wa timu umewaambia waanze kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo huo.

DOREFA imekuwa ikifanya mialiko ya mara kwa mara kwa miamba ya soka kucheza na timu hiyo ambayo wamedhamiria kuipandisha daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara wakati huu ambao makao makuu ya nchi yamehamia mkoani humo huku Wizara zote zikiwa tayari zimeshamia huko.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here