Home Kitaifa Ushindi wa Simba Arusha umeipeleka nusu fainali FA Cup

Ushindi wa Simba Arusha umeipeleka nusu fainali FA Cup

3539
0
SHARE

Simba Sport Club imekuwa timu ya pili msimu huu kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (FA Cup) baada ya jana Mbao FC kuwa timu ya kwanza kujihakikishia kucheza nusu fainali.

Bao lililoipa ushindi Simba limefungwa na Laudit Mavugo dakika ya 55 baada kupiga kichwa mpira ambao beki wa Madini alishindws kuumili wakati huohuo golikipa akawa amesogea kutoka golini kujaribu kuokoa Mavugo akajaza mpira kwenye kamba zilizokuwa tupu.

Simba ambao msimu uliopita waliishia robo fainali, wameifunga Madini FC kwa bao 1-0 huko jijini Arusha na kusonga mbele kwenye masgindano hayo ambayo bingwa wake ataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao.

Yanga vs Tanzania Prisons na Azam vs Ndanda ni mechi mbili za robo fainali zinazosubiriwa kutoa timu mbili zitakazoshinda na kuungana na Mbao FC pamoja na Simba katika hatua ya nusu fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here