Home Kitaifa Ulimwengu nje ya Taifa Stars

Ulimwengu nje ya Taifa Stars

4261
0
SHARE

Wakati timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’,kikitarajiwa kuingia kambini leo Machi 19, 2017 kwenye Hoteliya Urban Rose, Dar es Salaam, kikosi hicho cha Kocha Salum
Mayanga, kitamkosa Thomas Ulimwengu kutoka AFC Eskilstunaya Sweden.

Taarifa ambazo Mayanga amezipata kutoka Sweden ni kwamba Ulimwengu kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo ya AFC Eskilstuna. Hivyo sasa Mayanga atabaki na washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim
Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).

Mbali ya hao, nyota wengine aliowataja Jumatatu iliyopita ni walinda milango, Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).

Mayanga aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).

Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shiza Kichuya (Simba SC).

Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati wasaidizi wake ni Kocha Wa Makipa, Patrick Mwangata, Meneja wa timu, Danny Msangi, Mtunza Vifaa Ally Ruvu wakati Daktari wa timu atakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here