Home Kitaifa Shime bado anaamini katika JKT Ruvu

Shime bado anaamini katika JKT Ruvu

1478
0
SHARE

Zainabu Rajabu

TIMU ya JKT Ruvu ndiyo timu inayoburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa kukusanya pointi 20 na ili ijinasue ni lazima ishinde mechi tatu kati ya sita zilizobaki lakini iombe timu nyingine zilizo kwenye hatari hiyo zisishinde mechi zao.

Timu zilizo kwenye hatari hiyo ni Majimaji yenye pointi 22 na Toto Africans iliyojikusanyia pointi 25 ingawa timu nyingine pia zimepishana kwa pointi chache.

Akizungumza na Shaffihdauda.co.tz, Bakari Shime ambaye ni kocha mkuu wa Maafande hao ameonyesha kutokata tamaa kwani ana mipango ya ushindi kwenye mechi zao zilizobaki huku akitamka kuwa kipindi hiki cha mapumziko hakuna kulala na wameanza mazoezi kwenye Uwanja wao wa Mlalakuwa.

“Natumia nafasi hii ya mapumziko kufanya marekebisho ili tutakaporejea kwenye mechi zilizobaki tuweze kupambana na kuinusuru timu isishuke daraja, wachezaji wote wapo vizuri hakuna mwenye majeraha,” alisema Shime.

Endapo JKT Ruvu itashinda mechi tatu basi itafikisha pointi 29 ambazo
zinaweza kuwabakiza kwenye ligi kuu msimu ujao na si vinginevyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here