Home Kimataifa Nyie ongeeni tu ila Yaya Toure anamkubali sana Gurdiola

Nyie ongeeni tu ila Yaya Toure anamkubali sana Gurdiola

1773
0
SHARE

Pamoja na kutupwa nje katika mashindanonya Champions league, lakini bado tu Yaya Toure ana imani na Man City. Tofauti na watu wengine walivyopoteza imani katika klabu hiyo na kuanza kuibeza, Toure yupo tofauti nao na ni kama vile yeye anawabeza wanaoibeza.

Yaya Toure ambaye mwanzo wa msimu haukuwa mzuri kwake kutokana na matatizo baina yake na kocha wa timu hiyo Pep Gurdiola. Lakini kuonesha kuwa hana noma na Mhispania huyo Toure amemmwagia sifa Gurdiola na kusema kuwa bado ana imani naye.
Toure anaamini aina ya uchezajinwa Manchester City utawapa makombe mengi tofauti na watu wanavyofikiria “ukiangalia jinsi tunavyocheza na mbinu za mwalimu naamini inaweza kutuletea makombe,hata kama sio msimu huu lakini mbeleni tutapata.”
Kuhusu kupingwa kwa mbinu za Gurdiola, Yaya anasema “huwezi ukakwepa wapingaji,sio kila kitu kinakubalika kwa kila mtu na inapaswa uwe tayari kwa hilo,najua watu wanasubiri tufeli lakini sisi haitupasi kuangalia hivyo bali tufanye kazi kwa bidii sana”
Yaya Toure anasema wao kama Man City waala hawasikii kelele za watu wengine bali wanapambana tu,ameongezea kuwa timu yao inafurahia mfumo wa kocha wao na wala hawana mpango wa kubadilisha aina yao ya uchezaji.
Toka Pep Gurdiola ajiunge na Man City akitokea Bayern Munich, maneno na upinzani umekuwa mkubwa juu yake. Wengi wamekuwa wakipinga aina yake ya uchezaji wakidai inawafanya Man City waonekane wa kawaida sana,kutolewa katika Champions League kumeleta kelele nyingi zaidi lakini Toure bado anamkubali Pep.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here