Home Kimataifa Kumbe Pogba ana madeni,huwezi amini anayemdai ni nani

Kumbe Pogba ana madeni,huwezi amini anayemdai ni nani

17923
0
SHARE

Paul Pogba msimu huu alirudi Uingereza, lakini safari hii alikuja Uingereza kama mtu mzito sana tofauti na zamani alivyokuja. Mwanzoni Pogba aliwahi itumikia Man United lakini alikuwa kama kinda ila safari hii ni jina kubwa katika biashara ya soka.

Sasa sikoa hii,pamoja na mahela yote aliyonayo Paul Pogba lakini anadaiwa, moja kwa moja unaweza anza kuhisi pengine huyo mtu anayemdai Pogba atakuwa tajiri sana kiasi kwamba hata Paul hana uwezo wa kumlipa.
Kama na wewe umewaza hivyo utakuwa umekosea sana, anayemdai Paul Pogba ni Kondi Moyo,Kondi hana kazi nzuri wala kipato kizuri bali Kondi ni mbeba mizigo, wakati Paul akihamia United alihitaji watu wa kumsaidia kubeba mizigo na kuiingiza ndani kati ya watu hao alikuwa Kondi.
Lakini Pogba imemchukua miezi mitatu hadi sasa,Pogba alihamia kwenye jumba lake jipya la kifahari mwezi wa December, na Kondi analalamika sana kwa kuwa anaamini aliifanya kazi ya kumbebea vifaa vyake kwa moyo mweupe lakini hadi sasa hajapewa pesa yake.
“Pogba ni mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa, nakumbuka wakati anahamia kwake ile siku tulifanya kazi kwa moyo mweupeee tukiamini atatulipa ila hadi sasa huwezi amini sijalipwa pesa yangu” alisema Kondi.
Kinachomkera zaidi Kondi ni kwamba kiasi anachomdai Pogba ni £100 tu,pesa bayo Pogba anaiingiza ndani ya dakika 3. Mabosi wa Pogba walidai pesa hiyo iliwekwa bank lakini Kondi ameibuka na kusema sio kweli.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here