Home Kitaifa Kessy ameeleza benchi la Yanga lilivyotaka kumkatisha tamaa

Kessy ameeleza benchi la Yanga lilivyotaka kumkatisha tamaa

4701
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

BEKI wa pembeni wa Yanga, Hassan Kessy, amesema kipindi kile ambacho alikuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, alipunguza mazoezi yake binafsi kwa kile alichokuwa anaona ni kujichosha wakati akiwa hapewi nafasi.

Hivi karibuni Kessy alirejea kwenye kikosi cha kwanza cha Mzambia, George Lwandamina baada ya kusota kwenye benchi muda mrefu kabla ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara na nyingine mbili za kimataifa za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zanaco.

Shaffihdauda.co.tz ilipiga Story na Hassan Kessy ambaye amesema: “Nilikuwa nafanya mazoezi kujiweka sawa lakini ilifikia muda nikapunguza kufanya kutokana na kuwekwa benchi ikiwa naweza kucheza na siyo majeruhi.”

“Ninahitaji kujiongezea fiziki katika kipindi hiki ambacho tayari nina nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza ili kuisaidia timu yangu,” alisema Kessy.

Aidha mchezaji huyo wa zamani wa Simba amesema alichopanga hivi sasa kila siku atakuwa anafanya mazoezi ya binafsi ya gym na kukimbia barabarani kwa ajili ya kurejesha fiziki yake iliyopotea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here