Home Kimataifa Barua ya wazi kwa babu yangu Arsene Wenger.

Barua ya wazi kwa babu yangu Arsene Wenger.

3785
0
SHARE

Na Eric Martin

Shikamoo babu,natumaini unaendelea vizuri tu kwa kuwa mkataba wako uliosaini mwaka 2014 unaokufanya uwe kocha namba 4 kulipwa vizuri zaidi duniani unakupa unachotaka,lakini je sisi mashabiki tunapata tutakacho?Hapana.

Unalipwa mshahara mkubwa kuliko Antonio Conte,kuliko Zinedine Zidane lakini hakuna cha kutufurahisha unachotufanyia kila siku sisi tunachekwa,kila siku sisi tunazomewa,tuonee huruma babu tumechoshwa na hii hali.
Unajisifu kwamba wewe unaleta faida ya kifedha kwenye timu yetu,babu faida za kifedha sisi mashabiki tulio Tanzania tunafaidika nini?Sisi hatuhitaji fedha babu tunahitaji ndoo,tunahitaji medali,tupe kombe babu,kama umeshindwa ondoka.
Waswahili wanasema “muungwana akivuliwa nguo,sharti ainame”. Babu umevuliwa nguo cha ajabu huinami na sasa unadhalilika hadi watoto wadogo wakina West Bromich wanakuchungulia. Ulivuliwa nguo ulipopigwa zile 10 na ulipaswa kuchuchumaa kwa kukubali tu kuachia ngazi ila ona hujainama na sasa unachungiliwa babu,umekosa uungwana?”
Babu tumevumilia mengi,tulipigwa 8 na United unakumbuka?tukajipa moyo tukuvumilie tu,tukafungwa na Liverpool 5 upo tu, Chelsea wakatupiga 6 babu hauondoki, tumegeuzwa shamba la bibi kila mtu anakuja kuvuna kwetu.
Ona yule Josefu wa mtaa jirani hapo wa Manchester anakuita “bingwa wa kufeli” jamani babu natamani kulia,unadhalilika na sisi wajukuu zako tunadhalilika babu,tunakuomba ondoka tu jamani babu tunaumia.Josefu kaja kakukuta akabeba makombe,huyuu Muitalia Carlosi naye msimu wa kwanza tu ona anawapa wenzetu kombe, wewe upo tu na koti lako kubwaaa.
Mimi mjukuu wako nakuomba tu nkukumbushe tena ya kwamba “heri aibu kuliko fedheha”, kama kuaibika umeshaabika wewe na wajukuu zako na sasa fedheha iko mlangoni inabisha hodi, babu yangu naomba ondoka ili fedheha isikukute. Tutakukumbuka kwa mema uliyotutendea lakini sasa imetosha tunaomba uondoke.
Ni mimi mjukuu wako Erick Martin ukintafuta instagram andika Kicki_19,nakutakia kila la kheri huko uendako.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here