Home Kimataifa Bale naye kufuata nyayo za Wayne Rooney.

Bale naye kufuata nyayo za Wayne Rooney.

3844
0
SHARE

Hivi ushawahi kumuona Bale akiwa ana nywele fupi sanaa? nadhani ni nadra sana. Na je ushawahi kujiuliza kwanini Bale inamuwia ngumu kubadili style ya nywele zake wakati Ronaldo yeye anafanya hivyo karibia kila mechi?sasa sikia jibu liko hapa.

Gareth Bale na Wayne Rooney wote hawachekani, wakati Rooney akilipia kiasi kikubwa cha pesa ili kuotesha nywele zake, Bale yeye anazilazalaza ili kipara chake kisionekane. Ule muonekano wa nywele za Bale kuzilaza nyuma sio kwamba anaupenda sana ila anaficha upara.
Lakini sasa marafiki wa karibu wa Bale wanasema mcheza soka huyo amechoshwa na style yake ya nywele, na sas Bale anataka style mpya ila ugumu unaokuja kwake ni kwamba ataweka style gani ambayo nayo itamfichia upara wake?
Bale yeye alikuwa hataki kufanya kama alichofanya mchezaji mwenzake wa Wales Joe Ladley ambaye ilimgharimu £10,000 kuotesha nywele kwenye kichwa chake.Bale alikuwa hataki kuotesha bali anataka kutumia alizonazo kuziba upara huo,lakini sasa ameanza kubadili mawazo.
Ripoti zinasema Bale ameongea na Ladley akamuelekeza jinsi alivyopandikiza nywele zake na sasa yeye pia anafikiria kufanya hivo, lakini yeye anaogopa kufanya hivyo katikati ya msimu na hivyo itambidi kusubiri hadi mwezi wa 5.
Bale sasa anaweza kusafiri hadi Cardiff kukutana na madaktari maarufu wa masuala ya uoteshaji wa nywele(KSL HAIR).Bale amekuwa na aina hiyo hiyo ya nywele karibia msimu mzima sasa lakini msimu ujao tutarajie style mpya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here