Home Kimataifa Sababu 3 za kitaalam kwa nini Rojo alipewa ndizi katikati ya mechi

Sababu 3 za kitaalam kwa nini Rojo alipewa ndizi katikati ya mechi

30967
0
SHARE

Alhamisi iliyopita Manchester United ilicheza na Rostov katika mchezo wa Europa League kwenye uwanja wa Old Trafford na United kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0 na hatimaye kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa jumla ya magoli 2-1 baada ya sare ya kufungana goli 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Urusi.

Story kubwa kwenye mechi iliyochezwa Old Trafford ilikuwa ni beki wa Manchester United Marcos Rojo kupewa ndizi kutoka benchi la ufundi na kuila huku game ikiwa inaendelea. Mourinho alichukua ndizi na kumpa Young ambaye alimpa Jojo na kuila wakati mechi inaendelea.

Sasa Sports Extra kinachorushwa na Clouds FM kimefanya mazungumzo na Dr. Issac Maro kutaka kujua kwa kitaalam nini faida ya ndizi kwenye mwili hususan kwa wanamichezo na kwa nini Rojo alipewa ndizi wakati mechi bado inaendela.

Dr. Maro akafafanua kazi tatu muhimu za ndizi hususan kwa wanamichezo na kueleza kwa nini Rojo alipewa ndizi huku mechi ikiwa inaendelea.

“Ndizi moja inazaidi ya gram 30 za wanga ambao unahitajika kwa wanamichezo ili waweze kupata nguvu kuhakikisha misuli inaweza kufanya kazi kama kawaida. Inasaidia pia kwenye akili, kama akili haipati kiasi cha kutosha cha sukari na nguvu, maana yake haiwezi kufanya kazi,” anasema Dr. Isaac Maro.

“Ndizi pia ina kiwango kikubwa cha Potassium inayosaidia kwa kiasi kikubwa kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu na kuhakikisha muda wote kiwango cha sukari hakiwi kikubwa sana wala hakiwi kidogo sana na kumsaidia mtu kufanya kazi vizuri. Pia inakuwa kama madini chumvi ambayo yanasaidia kuweka maji mwilini kwahiyo unakuta mwanamichezo hapungukiwi na maji na kuwa na uwezo wa kufanya kazi muda mrefu.”

“Ndizi zina Vitamin C ambavyo ni muhimu sana, karibu asilimia 15 ambazo zinahitajika kwa siku zinaweza kupatikana kwenye ndizi moja mbivu , inasaidia sana kwenye kujenga misuli na kuhakikisha kinga inabaki juu na mambo yanaenda vizuri. Pia Vitamin C inasaidia kwenye uzalishaji na utoaji wa Adrenalin ambayo inatusaidia tuwe na nguvu na ku-perfom zaidi.”

Kama mchezaji alipewa ndizi basi walifanya vizuri kwa sababu itakuwa ilisaidia kumfanya a-focus zaidi na kuweza kucheza kwa muda mrefu zaidi bila kuchoka na baada ya hapo aweze kupumzika vizuri.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here