Home Kitaifa March 18, 2017 timu ya kwanza imefuzu nusu fainali FA Cup

March 18, 2017 timu ya kwanza imefuzu nusu fainali FA Cup

2779
0
SHARE

Robo fainali ya kwanza ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (FA Cup) imechezwa kwenye uwanja w Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera na kushuhudia wenyeji Kagera Sugar wakipoteza kwa bao 2-1 mbele ya Mbao FC kutoka Mwanza.

Mbao walianza kupata bao lao la kwanza kipindi cha kwanza likifungwa na Salum Idd kwa shuti kali la mita 29 kutoka golini lililomshinda golikipa wa Kagera Sugar Juma Kaseja.

Kipindi cha pili Kagera Sugar wakarudi kwa kasi na kulishambulia goli la Mbao wakitafuta bao la kusawazisha, wakati wakiwa katika harakati za kupata goli, Mbao wakafanya shumbulizi la kustukiza lililowapa bao la pili ambalo lilijazwa kambani na Dickson Ambundo aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi.

Muda ukiwa unayoyoma, Kagera walifanikiwa kupata gili la kufutia machozi likifungwa na Ame Ally ‘Zungu’ akiunganisha kwa shuti mpira uliopigwa na Mohamed Faki.

Mbao FC inakua timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya FA Cup msimu huu ikisubiri kucheza na timu zitakazo shinda kwenye michezo kati ya Simba vs Madini FC, Azam FC vs Ndanda FC na Tanzania Prisons vs Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here