Home Kimataifa Maneno ya kocha wa Zanaco kabla ya kuikabili Yanga nchini Zimbabwe

Maneno ya kocha wa Zanaco kabla ya kuikabili Yanga nchini Zimbabwe

10246
0
SHARE
Numba Mumamba (kushto) kocha mkuu Zanaco FC

Na Zainabu Rajabu

NI ZAIDI YA VITA, ndivyo unavyoweza kusema ndani ya klabu ya Zanaco, inayojiandaa kukabiliana na Yanga leo Jumamosi March 18, 2017 hii katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Shaffihdauda.co.tz ilizungumza na kocha mkuu wa mabingwa hao wa Zambia Numba Mumamba ambaye amesema wataingia uwanjani kuikabili Yanga wakiamini chochote kinaweza kutokea ndani ya ardhi yao.

“Hatutakiwi kubweteka licha ya kuwa tuna bao la ugenini, goli hilo linaweza kurudishwa mara moja kama Yanga wamekuja na mbinu mpya katika nchi yetu,” alisema Mumamba.

“Ikumbukwe makosa waliyofanya Yanga kuruhusu bao kwenye ardhi yao yanaweza kufanyika pia uapande wetu, inabidi tufanye kazi ya ziada kuhakikisha tunacheza kwa tahadhari, tusijione tumefanikiwa tupambane.”

Mshindi Wa mechi hiyo atasonga mbele kwenye hatua ya makundi ya ligi hiyo, huku atakayepoteza atapelekwa kucheza Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here