Home Kimataifa Hizi ni sababu 10 kwanini Kante anapendwa na kila mtu.

Hizi ni sababu 10 kwanini Kante anapendwa na kila mtu.

5597
0
SHARE

1.Amekuwa nyota kwa kila timu aliyochezea.Toka alipokuwa Leicester City mchango wake ulikuwa mkubwa sana na kuisaidia Leicester kubeba ubingwa.Amehamia Chelsea nako ni vivyo hivyo kwanj amewaweka uongozi wa ligi na amekuwa muhimu sana kwao.

2.Hana makuu.Kante ni mchezaji ambaye nje ya uwanja utamuona mshamba mshamba,hana mbwembwe za misuko sijui style za nywele,na anasema yeye baada ya mechi tu hurudi nyumbani kulala.
3.Alivyokuwa mhimili wa Leicester.Kwa timu ya Leicester kuchukua ubingwa wa Uingereza ilikuwa ndoto.Hii ni sababu ambayo kila timu inatamani kuwa na Kante wao,na ndio maana wakati wa usajili timu mbali mbali zilimpigania Kante.
4.Tabasamu lake.Kante ni mchezaji ambaye ni ngumu sana kukasirika na muda wote anaonekana na furaha.Wataalamu wa mambo ya soka wanasema kati ya kitu ambacho mashabiki wengi wanachofurahi kwa Kante tabsamu ni mojawapo.
5.Bado anakumbuka alipotoka.Baada ya kutoka Leicester City wengi walidhani ndio mwisho wa Kante na Leicester,lakini Kante bado ana mapenzi na Leicester.Katika ushindi wao dhidi ya Sevilla, Kante alikuwepo kuwashangilia Leicester wakitinga robo fainali ya UEFA.
6.Hakumsaliti Ranieri.Kabla ya kocha aliyewapa ubingwa Leicester City, Claudio Ranieri kutimuliwa kulikuwa na habari kwamba wachezaji wakubwa walimsaliti. Ryad Mahrez na Jamie Vardy ninmiongoni mwa majina makubwa ya wasaliti wa Ranieri. Lakini Ngolo Kante alikuwa swahiba wa Ranieri na hata katika mchezo kati ya Chelsea na Leicester City walionekana kufurahi pamoja.
7.Yeye utamuona tu uwanjani.Kante ni mtu ambaye hata shopping huwa haonekani sana. Muda wake mwingi huutumia nyumbani akitoka nyumbani ni mazoezini akitoka mazoezini ndani kupumzika.
8.Hakuwa gumzo miaka miwili iliyopita.Ni kama zero to hero,miaka miwili iliyopita hakuna mtu ambaye alikuwa akimzungumzia Kante. Miaka hiyo Kante alikuwa Cannas hakuwa na jina na hata kwenye Social medias lakini sasa yuko mdomoni mwa kila mtu.
9.Sio bishoo.Katika umri wake ni dhahiri kwamba alitakiwa awe bishoo kama Ozil,Pogba au Depay.Lakini Kante sio bishoo hata kidogo, ukimuangalia maisha yake utagundua anaishi kama mzee wakati yeye ni kijana.
10.Siku zinavyozidi kwenda ndiyo anakuwa gumzo.Wengine walidhani baada ya kuondoka Leicester City ingekuwa mwisho wake na asingeng’ara akiwa na Chelsea. Lakini msimu huu anaonekana anaenda tena kutengeneza historia mpya kwa kuwapa ubingwa Chelsea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here