Home Kimataifa Baada ya kuboronga,sasa Man City kutumia £200m kujijenga upya

Baada ya kuboronga,sasa Man City kutumia £200m kujijenga upya

2476
0
SHARE

Baada ya kutolewa katika Champions League na Monaco mabosi wa Man City wanaona timu yao haikustahili kutolewa katika hatua hiyo. Aina ya benchi la ufundi na wachezaji waliokuwa nao Man City wanaona walipaswa kushindana na Real Madrid na Barcelona katika mbio za ubingwa wa Champions League.

Manchester City wameshajaribu kutumia zaidi ya £80m kununua mabeki wawili tu wa kati(Otamendi na Stones),lakini bado safu yao ya ulinzi imekuwa nyanya na kufanya makosa yanayoigharimu timu. Wakati City akitolewa na Monaco mabeki wa City walizembea kuucheza mpira wa cross ambao Bakayoko aliuwahi na kupiga kichwa kilichoenda moja kwa moja wavuni.
Tatizo la mabeki linasemekana kumkosesha raha sana Gurdiola na sasa anatarajia kuingia sokoni kutumia kiasi kikubwa kutafuta mabeki awatakao. Inafahamika kwamba Kompany hana tatizo na alishapona majeruhi ila sasa hana furaha na timu na yupo tayari kuondoka, huku Sagna,Clichy na Zabaleta nao wakiwa karibuni kuondoka klabuni hapo.
Tayari Leornado Bonucci ni jina lililopo kwenye list ya Gurdiola, Bonucci amekuwa na msimu mzuri na Juventus kiasi cha kuvitamanisha vilabu vingi.Jina la beki wa kushoto wa Valencia Jose Gaya pia limo kwenye orodha ya Gurdiola na mlinzi wa kulia wa Bayern Munich Joshua Kimmich naye akiwa kwenye rada ya Gurdiola.
Sio mabeki tu ambao ni tatizo kwa Gurdiola kwani toka amuuze Joe Hart, Gurdiola amekuwa na tatizo jipya la kipa.Magolikipa wawili Caballero na Claudio Bravo wameigharimu sana Man City. Gurdiola anataka kujaribu kutafuta golikipa mmoja bora ili kutibu tatizo hilo ndani ya Manchester City.
Ripoti zinasema matajiri wa Man City wametenga kiasi cha £200m ili kuijenga tena Man City. City wataleta wachezaji wapya na kupungiza wachezaji wengi kuanzia ndani ya timu na wale walioko nje ya timu kwa mkopo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here