Home Kitaifa Maoni na mtazamo wa Waziri Nape Nnauye kuelekea uchaguzi wa CAF

Maoni na mtazamo wa Waziri Nape Nnauye kuelekea uchaguzi wa CAF

2147
0
SHARE

Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya uchaguzi wa rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Nape Nnauye ametoa mtazamo wake kuelekea uchaguzi huo.

Mh. Nauye amesema, anaamini Hayatou atashinda katika uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Ahmad Ahmad. Nauye pia amemtakia kila la heri Leodgar Tenga ambaye ni mtanzania anaegombea nafasi ya kuwa mjumbe wa baraza kuu la FIFA pamoja na chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) kinachoomba kujitegemea kutoka Tanzania na kuwa huru kisoka kama  nchi

“Uchaguzi huu unaweza kubadilisha historia ya soka nchini kwetu kwa mambo mawili. Jambo la kwanza, serikali tunaimani na Ledgar Chilla Tenga na tunamuunga mkono kwa nafasi aliyoiomba na yapo matumaini kwamba atafanya vizuri kwa sababu serikali imeangalia mambo yanavyokwenda, kwa hiyo Tenga akichaguliwa kuingia kwenye FIFA itakuwa ni maendeleo makubwa kwa upande wan chi yetu kwa upande wa mpira wa miguu,” alisema Nauye wakati akihojiwa kwenye kipindi cha michezo cha Sports Extra kinachorushwa na Clouds FM.

“Jambo la pili ni kwa muda mrefu Zanzibar imekuwa ikiomba kuwa mwanachama wa CAF, tunamatumaini kwamba tumefata hatua zote nap engine tunaweza tukapata habari njema kwamba Zanzibar imeruhusiwa kuwa mwanachama wa CAF na hili litamaliza mivutano iliyopo Tanzania bara na Zanzibar katika mambo mbalimbali kwenye michezo hasa mpira wa miguu.”

“Kwa hiyo haya mambo mawili makubwa tunaamini kwamba yatabadilisha historia ya mpira wa miguu katika nchi yetu. Na sisi kama serikali tunaunga mkono na tunawatakia kila la heri.”

“Sitegemei sana mabadiliko makubwakwenye nafasi ya uraisi wa CAF licha ya kuwepo na upinzani mkali kati ya Issa Hayatou na Ahmad Ahmad lakini nadhani Hayatou atarudi, ukiangalia amefanya kazi kwa muda mrefu na amekuwa na watu wengi wanaomuunga mkono. Nadhani huhu Ahmad ataleta changamoto na kama Hayatou atatumia vizuri hiyo Changamoto atafanya mageuzi makubwa ndani ya CAF lakini nadhani Hayatou atashinda.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here