Home Kimataifa Habari mpya kutoka Arsenal.

Habari mpya kutoka Arsenal.

26242
0
SHARE

Inafahamika kwamba Arsene Wenger ndio kocha wa kwanza kupiga hatua katika usajili wa Kylian Mbappe. Kabla hata watu hawajaanza kumzungumzia sana Mbappe,Wenger tayari alikwishaongea naye. Baada ya michezo miwili kati ya Monaco na Man City jina la Mbappe ndio limekuwa gumzo zaidi na watu kuelewa kwanini Wenger anamtaka. Sasa mashabiki wa klabu hiyo wametumia kurasa zao za twitter kuishinikiza klabu hiyo kumnunua Mfaransa huyo japo sasa watakabiliana na upinzani kutoka klabu zingine zinazomtaka.

Arsenal pia wamechungulia sehemu na kumuona mchezaji mwingine hatari sana ambaye ana umri mdogo na dunia haimzungumzii. Huyu ni kijana wa nchini Uturuki mwenye umri wa miaka 19 aitwaye Berkay Ozcan. Ozcan kwa sasa anaichezea Stuttgarts kwa sasa, mtandao mmoja wa michezo nchini Uturuki unasema Wenger ameshakutana na wakala wa Ozcan lakini kwa sasa Ozcan amedai kuelekeza nguvu zake kuisaidia Stuttgarts tu.

Naye James Whealling muandishi nguli wa masula ya michezo ameandika kwamba, wachezaji wa Arsenal wanatarajia kukosa mamilioni kama timu yao ikishindwa kufudhu kuingia nne bora ya ligi ya ligi ya Uingereza. Msimu uliopita UEFA waliipa Arsenal kiasi cha £47m baada ya kufudhu katika 16 bora ya michuano ya Champions League.

Mwisho ni Mesut Ozil,kumekuwa na tetesi kwamba siku za Ozil Arsenal zinahesabika. Ozil amekuwa kwenye mvutano kati yake na Arsenal kuhusiana na mkataba wake. Lakini sasa Ozil anaonekana kubaki Arsenal,japokuwa wako mashakani kushiriki Champions League msimu ujao Ozil amesema “siku moja natamani kuchukua Champions League nikiwa hapa na Arsenal” kauli ambayo imetafsiriwa kama kuzika tetesi za yeye kuihama Arsenal, tayari inasemekana Arsenal wameandaa mkataba mnono kwa ajili yake.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here