Home Kimataifa #Kuelekea uchaguzi wa CAF: Rais wa chama cha soka Zimbabwe awekwa mtu...

#Kuelekea uchaguzi wa CAF: Rais wa chama cha soka Zimbabwe awekwa mtu kati

1777
0
SHARE

Jana katika kikao cha kamati ya utendaji ya Caf iliyokutana Addis Ababa, Ethiopia, waliamua kwa pamoja kumpeleka kwenye kamati ya nidhamu rais wa chama cha soka Zimbabwe Philip Chiyangwa ambaye pia ni rais wa COSAFA.

Chiyangwa aliandaa party Harare, Zimbabwe na kuwaalika viongozi wengi wa vyama vya soka Afrika. CAF walimzuia kufanya hivyo lakini yeye akasema ametoa mialiko hiyo kwa jamaa zake wahudhurie kwenye tafrija ambayo yeye anasherekea birthday yake pamoja na ushindi alioupata mwezi December wa kuwa rais wa COSAFA.

Kimsingi,   Chiyangwa alikuwa anawaalika viongozi hao kuwavuta na kuwatengeneza kuelekea uchaguzi wa rais wa CAF kwa sababu yeye ndio campaign manager wa Bw. Ahmad Ahmad.

Katika mwaliko huo, alikuwepo pia rais wa FIFA Gianni Infantino ambaye pia alihudhuria, viongozi wengi ambao walialikwa hawakuhudhuria badala yake wakaenda wale ambao wanamuunga mkono Ahmad Ahmad.

CAF walimtahadharisha Chiyangwa kwamba, kama anawahusisha viongozi wa mataifa mengine ambao sio wanachama wa COSAFA, mkutano huo utakuwa ni batili kwa sababu hauendani na taratibu za CAF. Chiyangwa akapuuza na kuhoji ulipo uhalali way eye kuwekewa mipaka na kuchaguliwa watu wa kushrekea nae siku yake ya kuzaliwa.

Mkutano ukaendelea, sasa kutokana na kukiuka maagizo ya CAF, jana kamati ya utendaji ikaamua kwa pamoja kuwa Chiyangwa aende kwenye kamati ya nidhamu ya CAF ili aweze kushughulikiwa.

Infantino baada ya kuja Afrika (Afrika Kusini) ambapo alikutana na wenyeviti wote wa vyama vya soka barani Afrika alisema ziara hiyo ni ya kawaida katika kutembelea vyama vya michezo mabara mbalimbali kufatilia changamoto zao na kuzijua.

Baada ya hapo akaanza kuzitembelea nchi ambazo zilikuwa zinaonekana hazimuungi mkono moja kwa moja Ahmad Ahma nchi kama Uganda na Rwanda. Akazitembelea na kukutana na viongozi wa soka kuweka mazingira mazuri kwa Ahmad Ahmad.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here