Home Ligi EPL Conte: Hazard Hakucheza Kwa Dakika 25 Kwa Sababu Alikuwa Anapigwa Mateke Tu.

Conte: Hazard Hakucheza Kwa Dakika 25 Kwa Sababu Alikuwa Anapigwa Mateke Tu.

4209
0
SHARE
Chelsea manager Antonio Conte shanks hands with Chelsea's Eden Hazard during the EPL Premier League match between Chelsea and Tottenham Hotspur at Stamford Bridge, London, England on 26 November 2016. (Photo by Kieran Galvin/NurPhoto via Getty Images)

Antonio Conte alimsifia Eden Hazard kwa kuwa muungwana kwenye mchezo dhidi ya Manchester United baada ya kushuhudia dakika ambazo Conte ameziita “dakika 25 za kubutuliwa au kupigwa mateke” katika mchezo ambao Chelsea ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye robo fainali ya komba la FA.

Hazard alifanyiwa faulo katika dakika za mwanzo akijikuta anakwatuliwa mara kadhaa kwenye mchezo wa siku ya Jumatatu ikiwa ni mbinu iliyoonekana kutumiwa na Manchester United kupunguza uwezo wake mchezoni. Katika mchezo huo Phil Jones alionekana kupewa Jukumu la kumchunga huku Ander Herrera akijikuta katika wakati wa kupokea kadi mbili za njano kutoka kwake.

Conte alionyesha wazi kukerwa na namna ambayo Manchester United walikuwa wakicheza dhidi ya Eden Hazard akiwa katika eneo lake la ufundi, huku wakijibizana na kocha Jose Mourinho katika nyakati tofauti, na baada ya mchezo kocha huyo wa Chelsea alimsifu mchezaji wake huyo kwa kutokujishughulisha ama kujali mbinu walizokuja nazo United kwa kumchezea kwa nguvu.

“Fikra zangu ni hizi: wanatakiwa kucheza mpira, na wachezaji wangu wanataka kucheza mpira,” Conte alisisitiza.

“Kwa dakika 20 au 25 ilikuwa haiwezekani kwa Hazard kucheza mpira. Nilichoona ni kuwa alijikuta anapigwa mateke tu. Sidhani kama mimi ni mwendawazimu lakini nilimwona yeye peke yake akiwa katika wakati huo.

“Hili ni jibu langu kwa swali. Hazard, kwa dakika 25, asingeweza kucheza kwa sababu alikuwa anapigwa mateke tu.

“Alionyesha kuwa muungwana sana. Mtu asiyetikisika kirahisi. Ni ngumu na hatari sana kupigwa au kukwatuliwa kutokea nyuma. Lakini aliendelea kuwa muungwana. Najua kuwa wengi wanaweza kushangazwa na uungwana wake.

“Najifunza kuendelea kumfahamu vyema msimu huu unavyoendelea, na naweza kusema ni mtu mwenye tabia ya kipekee, nimejifunza hilo”

Alipoulizwa kama Manchester United waliamua kwa makusudi kuwa wanamkwatua Hazard, Conte alijibu kuwa “sifahamu lakini mbinu hii ya kucheza kwa kwenda kumpiga teke/kumkwatua mpinzani haipo. Sio mpira wa miguu kwa upande wangu. Sidhani kama hii inaweza kuwa mbinu. Huu ndo ukweli.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here