Home Kitaifa Bocco bado anauota ubingwa wa VPL 2016/17

Bocco bado anauota ubingwa wa VPL 2016/17

2423
0
SHARE
John Bocco 'Adebayor'-Nahodha wa Azam FC

Zainabu Rajabu

NAHODHA wa Azam FC, John Bocco amesema wataingia kwenye mbio za kupigania ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuifunga Yanga kwenye mchezo wa marudiano.

Azam FC na Yanga zinatarajia kurudiana wiki tatu zijazo kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Shaffihdauda.co.tz ilipiga stori Bocco ambae amesema hawatokuwa wateja kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu msimu huu.

Watahakikisha wanaifunga Yanga ili kuikimbiza Simba iliyopo kileleni mwa Ligi na wanamatumaini ya kupata ushindi kutokana na kikosi chao kuamka na kuanza kufanya vizuri,” – Bocco

Aidha, nahodha huyo amesema kocha wao wa sasa, raia wa Romania ni mzuri  na anaeleweka kwa wachezaji ukilinganisha na ilivyokua kwa Zeben Hernandez aliyetimuliwa.

Azam inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 44 pointi tisa nyuma ya Yanga yenye pointi 53 lakini Azam imeachwa kwa pointi 11 na Simba ambao ndio wanaongoza ligi hadi sasa baada ya timu hizo tatu kucheza mechi 24 kila moja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here