Home Kimataifa Mtambue Mzee Zaidi Kufunga Bao Kwenye Mechi Rasmi.

Mtambue Mzee Zaidi Kufunga Bao Kwenye Mechi Rasmi.

3044
0
SHARE

Inawezekana kuwa mchezaji Essam El-Hadary aliweka rekodi ya kuwa mtu mzima zaidi kucheza kwenye michuano ya AFCON akiwa na miaka 44 lakini bado kuna wachezaji wakubwa kumzidi wanaosaka mkate kupitia soka.

Mchezaji Kazuyoshi Miura ameweka rekodi ya kufunga goli katika klabu ya Yokohoma FCkwenye ushindi wa bao 1-0  kwenye ligi ya Japan maarufu kama J-League daraja la 2 dhidi ya Thespa Kusatsu akiwa na umri wa miaka 50 na siku 14.

“Nilikuwa na hamu ya goli na nilijaribu muda wote kuwa na fikra chanya,” alisema mchezaji na mshambuliaji huyo wa zamani wa nchi ya Japan.

Miura, ambaye alifunga mabao 55 kwenye michezo 89 ya nchi yake, alisaini mkataba mpya na klabu ya  Yokohama FC mwezi Januari.

Mchezaji huyu alianza maisha yake nchini Brazil na klabu ya Santos akicheza mchezo wake wa kwanza wa kulipwa mwaka 1986, huku pia akicheza katika ligi za Italia kwenye klabu ya  Genoa na kwenye ligi ya Croatia katika klabu ya Dinamo Zagreb kwenye miaka ya1990.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Yokohama mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 38.

Shirikisho la soka duniani, Fifa limeshindwa kuthibitisha kama Miura ndio mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga bao kwenye mechi rasmi.

Mtu mzima zaidi kufunga bao kwenye mechi za kimataifa ni  Billy Meredith, aliyeifungia Wales dhidi ya timu ya taifa ya England akiwa na umri wa miaka 45 na siku 73 mwaka 1919.

Pia aliifungia klabu ya Manchester City dhidi ya Brighton kwenye kombe la FA akiwa na umri wa miaka  49 na siku 208 mwaka 1924.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here