Home Kimataifa Kwa mara ya pili katika historia,El Classico kupigwa nje ya Hispania.

Kwa mara ya pili katika historia,El Classico kupigwa nje ya Hispania.

22111
0
SHARE

Kwa mara ya kwanza nchini Marekani miamba ya Hispania timu za Real Madrid na Barcelona zitakutana. Siku ya Ijumaa jambo hilo limetangazwa kwamba katika sehemu ya mashindano ya International Champions Cup (ICC), hiyo itakuwa July mwaka huu.

Hii itakuwa mara ya pili kwa El Classico kuchezwa nje ya Hispania. Miaka 34 iliyopita Real Madrid na Barcelona walikutana nchini Venezuela. Timu hizi zitakutana Jully 29 na inaonekana itakuwa kivutio kwa watu wengi duniani kufika katika mji wa Miami ambapo ndipo pambano hilo litapigwa.
Lakini wakati miamba hiyo ikijiandaa kukutana mjini Miami mwezi Julai, wikiendi hii ilishuhudiwa Barcelona wakipoteza mchezo wao dhidi ya Drportivo La Coruna. Barcelona walioonekana kuchoka sana katika mchezo huo walikubali kipigo cha bao 2-1.Kipigo hicho kinauweka ubingwa wao rehani kwani wapinzani wao wakubwa Real Madrid wanaonekana kuja kwa kasi.
Wakati Barcelona wakipigwa, mahasimu wao wakubwa Real Madrid waliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 2 kwa 1. Ushindi huo unawaweka Madrid kileleni wakiwa na alama 62 huku Barcelona wakiwafuata wakiwa na alama 60 na mchezo mmoja zaidi. Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 210 katika uwanja wa Santiago Bernabeu na kuweka rekodi ya mchezaji mwenye magoli mengi zaidi uwanjani hapo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here