Home Kimataifa Kura 100,000 zapigwa kutaka Brcelona na Psg warudiane,refa aliwatukana Psg.

Kura 100,000 zapigwa kutaka Brcelona na Psg warudiane,refa aliwatukana Psg.

28889
0
SHARE

Baada ya ushindi wa Barcelona wa mabao 6 kwa 1 dhidi ya PSG mengi yamezungumzwa.Kumekuwa na mambo mengi yakizungumzwa wengine wakiusifu uwezo wa Barcelona huku wengine wakiponda.Wengi wanasema Barcelona walibebwa mno katika mchezo huo ndio maana walishinda,penati walizopewa na penati waliyonyimwa PSG inazidi kuwaaminisha watu kwamba Barca walibebwa.

Sasa sikia hii,unaambiwa kumepigwa kura 100,000 ndani ya masaa 24 baada ya mchezo huo zikipendekeza mchezo huo urudiwe.Ishu ilikuwa hivi baada ya ushindi huo wa Barcelona muandishi mmoja aitwaye Luis Melendo aliandika “Napendekeza mchezo kati ya Barcelona na PSG urudiwe,naandika hivi kutokana na maamuzi mabovu ya refarii bwana Deniz Ayketin” baada ya Melendo kuandika hivyo aliiweka kwenye mtandao maarufu uitwao Change.Org.
 Melendo hakuishia hapo aliandika baadhi ya sababu anazoamini Barca walibebwa.Baada ya kuandika hivyo unaambiwa watu zaidi ya 100,000 waliweka sahihi zao kwamba wanaafikiana na Malendo na kupendekeza mchezo huo urudiwe.Ni jambl gumu na lisilowezekana kwa mchezo huo kurudiwa lakini hii inaonesha wazi kwamba mashabiki wengi wa soka hawajafurahishwa na alichofanya Ayketin katika mchezo huo.
Wakati hayo yakiendelea jipya lingine limeibuka kuhusu muamuzi wa mchezo huo.Inasemekana wakati wachezaji wa PSG walipojaribu kubishana na muamuzi huyo kuhusiana na maamuzi yake,muamizi huyo aliwatukana wachezaji hao kwa kuwaambia “f*ck you”.Jarida moja nchini Ufaransa limechapisha makala inayosema muamuzi huyo alishindwa kuzuia hasira zake hadi kuamua kuwatukana wachezaji.Mmiliki wa PSG Nasser El Khalaifi naye hakuwa nyuma kwani amejitokeza hadharani kumshambulia muamuzi huyo.
“Huwezi kufanya lolote kwa sasa kwani imeshatokea,lakini ni wazi unaona bila muamuzi tungekuwa na matokeo tofauti na haya.Unaweza ukaona wazi faulu aliyofanyiwa Di Maria lakini vilevile unaweza pata mashaka kuhusiana na ile penati ya Suarez,haikuwa sahihi” alisema Nasser.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here