Home Kitaifa Maneno ya Mavugo kwa mashabiki kuhusu ubingwa wa VPL

Maneno ya Mavugo kwa mashabiki kuhusu ubingwa wa VPL

8140
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

MSHAMBULIAJI wa Simba Laudit Mavugo, amesema wamepanga kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizobaki ili waweze kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Simba sasa hivi inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 55 na nyuma yake wapo Yanga wenye alama 53 na wote wamecheza mechi 24.

Mavugo ameiambia shaffihdauda.co.tz kuwa, wamejipanga kuhakikisha wanajituma kwa nguvu zote uwanjani ili wafanikiwe kupata ushindi katika michezo yote sita iliyobaki.

“Tunahitaji kushinda mechi zote zilizobaki ili kuweza kutimiza lengo letu kwani dhamira yetu ni ileile ya kutwaa ubingwa msimu huu, hivyo tunahitaji kuungana katika kipindi hiki cha mwisho kwa kuendelea kuimarisha umoja wetu kuanzia wachezaji, viongozi na mashabiki kwa ujumla,” alisema Mavugo.

Simba wanahaha kuhakikisha wanatwaa ubingwa huo ambao mara ya mwisho kuutwaa ilikuwa ni msimu wa 2011/12.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here