Home Kimataifa ‘Nilikuwa natafuta goli la Europa League kuliko kitu chochote’ -Samatta

‘Nilikuwa natafuta goli la Europa League kuliko kitu chochote’ -Samatta

9740
0
SHARE

Baada ya Mbwana Samatta kuifungia magoli mawili timu yake ya Genk kwenye mashindano ya Europa League na kuisidia kupata ushindi wa magoli 5-2 ugenini dhidi ya Gent, Samatta amesema alikuwa anatafuta kufunga goli kwenye michuano hiyo kuliko kitu chochote kwa hiyo magoli hayo mawili yamekuja katika wakati muafaka.

“Nakosa kitu cha kusema ni jinsi gani nilivyojisikia kwa sababu nilikuwa natafuta hilo goli la Europa kuliko kitu chochote nilikuwa nahangaika, na kipindi nalitafuta hayo magoli yalikuwa hayaji, kwa hiyo hadi inafika ile game nilikuwa nimeshahangaika sana kutafuta magoli na magoli yenyewesipati. Nilikuwa natumia kila njia hadi nikaamua ku-relax na kuondoa hicho kitu ili mwili wangu utulie nifanye kazi kama inavyotakiwa,” anasema Samatta wakati akihojiwa na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.

“Ilifika kipindi nikasema kama goli likija basi Mungu atakuwa ameleta baraka zake na lisipokuja basi kwa sababu nilikuwa naona kila napojaribu kulazimisha ndio nazidi kuumia na kwa sababu nachokitaka hakiji, nikaamua kumuachia Mungu, mimi nifanye kazi, kweli Mungu akaleta neema kwenye ile game. Nnadhani kikosi kilikuwa kizuri na mimi nilikua vizuri pia na nafasi zilikuwa zinapatikana.”

Magoli mawili aliyofunga Samatta kwenye mechi ya Europa League dhidi ya Gent yanamfanya kufikisha magoli manne kwenye michuano hiyo huku akiwa tayari amefikisha magoli 16 katika mashindano yote

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here