Home Kimataifa Refa wa Barcelona Vs PSG, Kukutana na Rungu La Uefa.

Refa wa Barcelona Vs PSG, Kukutana na Rungu La Uefa.

9119
0
SHARE

Barcelona waliweka kumbukumbu itakayodumu kwenye vichwa vya watu kwa siku nyingi zijazo na pengine ikachukua miongo kujirudia baada ya kutoka kufungwa mchezo wa kwanza kwa mabao 4-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 katika mchezo wa pili.

Barcelona waliruhusu goli ugenini lililotoa kila mwanga kuwa wasingeweza kufuzu kwa hatua inayofuata lakini waliibuka wakiongozwa na Neymar na kufunga mabao 3 katika dakika 7 za mwisho na hatimaye kufuzu.

Neymar alifunga mpira wa adhabu kwa ustadi dakika ya 88 ambapo iliwachangamsha Barcelona kabla ya kufunga mkwaju wa penalty na baadae Barcelona kufunga bao la ushindi katika dakika ya 95.

Lakini kumeibuka maswali mengi kuhusiana na adhabu za penalty hasa penalty iliyosababishwa na Luis Suarez ambayo iliwaweka Barcelona katika nafasi ya kutafuta bao moja tu ili waweze kufuzu. Penalty ile ilionekana kuwa na mgusano mdogo sana kati ya Suarez na beki Marquinhos ambapo Suarez alionekana kwenda chini kirahisi kupindukia.

Aytekin ambaye ndiye aliyekuwa mwamuzi wa mchezo huo alionyesha ishara ya adhabu hiyo huku akibishana na wachezaji wa  PSG waliokuwa wanamkumbusha kitendo kama hicho cha kujiangusha ambacho kilimsababishia Suarez kupata kadi ya njano.

Mwamuzi aliwasiliana na msaidizi wake wa nyuma ya goli ingawa alikuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuona tukio na kuwa karibu na tukio zima lilivyotokea.

Mjerumani huyo sasa inasemekana ataondolewa kwenye ratiba ya michezo ya klabu bingwa barani Ulaya na hatopewa nafasi ya kuchezesha mchezo wowote mkubwa msimu huu.

Jarida la Marca limeripoti kuwa Aytekin anaweza kushushwa zaidi kwenye mechi za chache na ligi za chini na kukiwa na uwezekano pia akasimamishwa kuchezesha michezo huku UEFA ikiwa inasubiri mambo yatulie.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here