Home Kimataifa Yaliyomkuta Tupatupa na Arsenal, yamkuta Shaffih Dauda na Barcelona.

Yaliyomkuta Tupatupa na Arsenal, yamkuta Shaffih Dauda na Barcelona.

24764
0
SHARE

Ni maajabu lakini ni kweli hivyo ndivyo unavyoweza kusema, sio wewe tu bali hata bwana Shaffih Dauda mchambuzi nguli wa soka Tanzania aliamini Barca asingeweza kutoka.Katika moja ya vipindi vyake vya Sports Xtra Shaffih amewahi kuahidi kutoa saa yake ya gharama kwa mtangazaji mwenzake Edgar Kibwana endapo Barcelona wangemng’oa PSG.

 Sasa magoli ya Lioneil Messi, Sergio Roberto, Luis Suarez na Neymar yanaenda kumvua bwana Shaffih saa yake. Ni mchezo ambao hata Barcelona wenyewe hawaamini na kupitia ukurasa wao wa Twitter wameandika “ulikuwa muujiza”. Hakuna aliyetarajia Barcelona wangeweza kuingia katika hatua ya robo fainali ya UEFA lakini ndio imeshatokea.
Baaada ya mechi ya kwanza kuisha kwa goli 4-0, alikuwa ni Luis Suarez na goli la kujifunga la Layvin lilizifanya timu hizi kwenda mapumzikoni kwa goli 2-0. Lakini kipindi cha pili Messi aliifungia tena Barcelona kabla ya Cavanni naye kufunga na kuifanya mechi izidi kuwa ngumu kwa Barcelona. Huezi kuamini hadi inafika dakika ya 88 zikiwa ni dakika 12 zimebaki ili mchezo uishe Barca walipaswa kufunga goli 3 ili kufuzu na goli hizo wazifunge ndani ya sekunde 660.
Dakika ya 88 free kick ya Neymar ilikwenda wavuni lakini bado ikawa inaonekana ni ngumu kwa Barcelona kuongeza goli zingine mbili. Baadae kidogo Barcelona walipata penati na Neymar kufunga, sub iliyofanywa na kocha Enrique ya kumuingiza Sergio Roberto ndio imeenda kuwapa Barcelona ushindi. Goli la dakika ya mwisho la Roberto ndilo limeivusha Barcelona.
Hii ni mara ya kwanza katika mashindano ya Champions league timu inafungwa goli 4-0 katila mechi ya kwanza na baadae mechi ya pili wanapindua matokeo. Ushindi huu umewafanya mashabiki wengi duniani kuumizwa kwani walibet kuhusu Barcelona kuondolewa. Inasubiriwa kuona kama Shaffih naye atavua saa yake au laa.“““““““““““““`

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here