Home Kimataifa Pique Aomba Ongezeko La Wauguzi. Usiku Wa Jana Utaleta Watoto Wengi.

Pique Aomba Ongezeko La Wauguzi. Usiku Wa Jana Utaleta Watoto Wengi.

4043
0
SHARE

GERARD PIQUE ameziomba mamlaka za afya na hospitali za Barcelona kuajiri wauguzi wapya na madkatari wa ziada kwa sababu miezi 9 kuanzia jana kutakuwa na ongezeko kubwa la watoto watakaozaliwa.

Barcelona jana walifanya moja ya mambo ambayo dunia haikuwahi kupata kuyashuhudia kwenye mchezo wa soka kwa kugeuza matokeo ya mabao 4-0 waliyofungwa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Paris St Germain na kushinda mabao 6-1 katika mchezo wa pili hivyo kufuzu kwa tofauti ya mabao 6-5 kwenye uwanja wa Camp Nou.

Zikiwa zimepita dakika 88 kwenye saa ya mwamuzi, Barcelona walikuwa wakihitaji kufunga mabao 3 ili waendelee, ndipo ambapo mchezaji Neymar alipoamua kufanya kila lililokuwa kwenye uwezo wake kuamua matokeo ya mchezo huo.

Na mchezaji Pique alikiri kuwa huu utabaki kuwa usiku wa kipekee kwenye historia ya klabu hiyo huku akisisitiza kuwa ni bora zaidi ya goli la Iniesta dhidi ya Chelsea mwaka 2009.

Pique alisema: “Nakumbuka goli la [Andres] Iniesta kwenye uwanja wa Stamford Bridge, lakini hili lililotokea hapa halifananishiki.

“Jambo moja ni kufunga goli muhimu katika dakika 5 za mwisho lakini hili jingine ni kufunga mabao 3 kwenye dakika 7.

“Unaweza kuiita kuwa ni maajabu, ni kipande muhimu kwenye historia.

“Tutasherekea usiku wa leo, ingawa tuna mazoezi siku ya kesho.

“Natumaini kuwa mahospitali yataongeza wauguzi kwani kwa miezi tisa ijayo kutakuwa na watoto wengi, na hii ni kwa sababu usiku wa leo utakuwa usiku wa mapenzi na wapendanao.”

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here