Home Kimataifa Alichokisema kocha wa PSG baada ya kufanyiwa fedheha Nou Camp

Alichokisema kocha wa PSG baada ya kufanyiwa fedheha Nou Camp

22896
0
SHARE

Kocha mkuu wa PSG Unai Emery alichanganyikiwa baada ya mechi ya marejeano dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wa Nou Camp kufatia kuchapwa bao 6-1 na kuondoshwa kwenye mashindano ya UEFA Champions League hatua ya 16 bora.

Goli la Edinson Cavani ambalo lilionekana kumaliza matumaini ya Barca kusonga mbele baada ya kuzidisha mzigo wa magoli matatu kwa miamba hiyo ya Hispania lakini bado haikuwa kikwazo kwao kufuzu kwenda robo fainali.

Lakini PSG waliachwa kwenye darasa la kujifunza kwenye michuano ya mabingwa wa Ulaya.

“Kwa kila mmoja ndani ya Paris Saint-Germain, viongozi, wachezaji pamoja na mashabiki hii ilikuwa ni siku mbaya kwao. Kilichotokea uwanjani ni kitu ambacho hakuwahi kukipitia,” alisema Emery.

“Tumepoteza nafasi nzuri ya kusonga mbele. Tulitaka kukua kulingana na mchezo, kipindi cha kwanza hatukucheza kwa kiwango tulichotaka. Tulitaka kucheza kama mchezo wa kwanza, tulitaka kucheza mtindo wa counter-attack. Baada ya goli la tatu timu ilikuwa vizuri, tulihitaji kupata matokeo mazuri kwa kufunga goli la pili.”

“Ndani ya dakika tano, tulipoteza kila kitu. Hatukuwa na uwezo wa kujilinda. Ni experience mbaya kwetu, lakini ni somo. Najifunza kupitia kushindwa, ni wazi tumepoteza fursa nzuri.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here