Home Kimataifa Timu 5 zilizowahi kutolewa klabu bingwa Ulaya kwa idadi kubwa ya magoli

Timu 5 zilizowahi kutolewa klabu bingwa Ulaya kwa idadi kubwa ya magoli

15554
0
SHARE

Story kubwa kwenye anga la michezo ni kuhusu kichapo walichopewa Arsenal na Bayern Munich kwenye mchezo wao wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya. Kwenye mitandao ya kijamii mijadala mingi ni kuhusu matokeo ya usiku wa March 7, 2017 ambapo rekodi nyingi zimewekwa.

Matokeo ya Arsenal kuondoshwa katika michuano ya Champions League kwa magoli 10-2 unaweza kuona ndio matokeo yenye magoli makubwa zaidi katika michuano hiyo. Lakini kuna matokeo mengine ni ya kushangaza kuliko hata hayo na mengine yanafanana na hayo.

Kutana na vipigo vikubwa vitano na timu ambazo zimewahi kuondolewa kwenye Champions League kwa idadi kubwa ya magoli katika hatua ya 16 bora katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Bayern Munich 12-1 Lisbon (2009) hatua ya 16 bora

Bayern Munich 10-2 Arsenal (2017) hatua ya 16 bora

Barcelona 10-2 Liverkusen (2012) hatua ya 16 bora

Lyon 10-2 Werder Bremen (2005) hatua ya 16 bora

Real Madrid 9-2 Schalke (2014) hatua ya 16 bora

Bayern Munich imeshinda 5-1 kwenye kila mchezo iliokutana na Arsenal kwenye hatua ya 16 bora, katika mechi tatu zilizopita kati ya Arsenal na Bayern Munich, Arsenal imepoteza mechi zote kwa idadi sawa ya magoli (5-1)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here