Home Kimataifa Kisa Arsenal, mtangazaji wa Clouds TV amenyolewa

Kisa Arsenal, mtangazaji wa Clouds TV amenyolewa

18020
0
SHARE

Kweli Arsenal usiiwekee dhamana, imepelekea shabiki wake kunyolewa nywele hadharani tena kama haitoshi mbele ya camera za Clouds TV.

Mtangazaji wa Clouds Media Group James Tupatupa amenyolewa nywele baada ya Arsenal kutupwa nje ya michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.

Baada ya game ya kwanza ugenini (Allianz Arena) ambapo Arsenal ilipoteza kwa kufungwa mabao 5-1 mbele ya Bayern Munich, Tupatupa alikua na matumaini makubwa kuwa The Gunners watasonga mbele kwa kuitoa Bayern kwenye mchezo wa marudiano.

Mtangazaji huyo wa anayetamba na segment ya ‘mtaa wa tatu’ ndani ya Sports Extra aliahidi kunyoa nywele zake za kichwani endapo Arsenal itatolewa kwenye mashindano hayo baada ya mchezo wa pili.

Sasa usiku wa Jumanne March 7, 2017 Arsenal ilipoteza kwa kupigwa goli 5-1 na kufanya kuondolewa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya magoli 10-2.

Leo asubuhi kwenye kipindi cha Clouds 360 ndani ya Clouds TV, Shaffih Dauda na Sam Sasali wamemnyoa Tupatupa ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake aliyoitoa majuma mawili yaliyopita.

James Tupatupa ni shabiki wa Arsenal wa wazi asiyeficha mahaba yake kwa klabu hiyo inayonolewa na Arsene Wenger.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here