Home Kimataifa Xavi Aweka Wazi. Anawafukuzia Guardiola na Enrique.

Xavi Aweka Wazi. Anawafukuzia Guardiola na Enrique.

3186
0
SHARE

Nyota wa zamani na nguli wa klabu ya Barcelona,  Xavi Hernandez ameweka bayana nia yake ya dhat ya kuja kuwa kocha wa klabu ya Barcelona baadae. Mchezaji huyo amesema anatamani kuja kufuata nyayo za makocha waliofanikiwa katika klabu hiyo na ambayo waliwahi kuichezea hapo kabla  Pep Guardiola na Luis Enrique ili apate kuifundisha siku moja.

Xavi alikuwepo na aliisaidia klabu ya Barcelona kushinda mataji 3 ya La Liga huku ia akitwaa mara mbili taji la klabu bingwa Ulaya two chini ya utawala uliotikisa dunia kwa miaka 4 wa Guardiola.

Lakini pia alifanikiwa kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya na pia ubingwa wa La Liga akiwa chini ya kocha Luis Enrique katika msimu wake wa mwisho kabla hajatimkia Qatari kuchezea klabu ya Al-Sadd mwaka 2015.

Mchezaji huyo amepanga kucheza mpaka mwaka 2018 kabla hajaamua kutundika daruga na kuamua kukimbiza ndoto zake hizo.

“Mpango wakweli ni kufika Barcelona nikiwa kama kocha,” alisema. “Huwezi kufahamu nini kitatokea, hivyo inabaki kuwa juu yangu.

“Inategemea pia na kipi ambacho unaamini unaweza kufanya, hali iliyopo, wakati wenyewe, na changamoto zilizopo. Lakini lengo langu, ninachotaka kufanya, hakuna kingine ni kufanya kazi na klabu ya FC Barcelona.”

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania anafanya kazi ya uchezaji na ukocha kwa wakati mmoja nchini Qatar na timu ya taifa hilo ya chini ya miaka 23 na ameweka wazi kuwa maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2022 ni mpango wa kuvutia.

Xavi ameweka wazi kuwa ni mfuasi na muumini mkubwa wa akili na filisofia ya soka iliyowekwa na aliyekuwa gwiji na kocha wa zamani wa Barcelona, marehemu Johan Cruyff, na kuongeza kuwa hajawahi kuwa mpenzi wa mchezo wa kushambulia kwa kushitukiza wa Diego Simeone akiwa Atletico Madrid.

Pamoja na hayo kamsifia Simeone kuwa naye ni kipaji chake na sio rahisi kufanya na kikubwa zaidi ni kuwa amewafanya wachezaji wake wafurahie kucheza hivyo na ni jambo la maana.

Ameongeza pia kuwa alikuwa angefurahia kucheza na Real Madrid iliyokuwa chini ya Zinedine Zidane, akisema: “Timu yake ikiwa na mpira napenda sana.

“Sio mpira wenye mambo mengi, anaenda mbele moja kwa moja na wanashambulia vyema kutokea katikati na mbele, huku mabeki wa pembeni wakiongeza nguvu zaidi.”

“Kwenye eneo la ulinzi, nahisi anacheza Kiitaliano zaidi kwa sababu amekulia huko.”

Ameweka bayana pia kuwa kilichowafanya Barcelona kuwa wa kipekee ni uwepo waLionel Messi, akielezea kuwa: “sidhani kama atatokea mwingine kama yeye.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here