Home Kimataifa Luis Enrique: Kama PSG Walifunga Mabao 4, Tunaweza Kufunga 6

Luis Enrique: Kama PSG Walifunga Mabao 4, Tunaweza Kufunga 6

7231
0
SHARE

Barcelona wamekuwa katika kiwango bora hasa kwenye safu yao ya ushambuliaji ambayo inampa kiburi na imani kocha wa klabu hiyo Luis Enrique kuamini kuwa wanaweza kuiondoa klabu ya Paris Saint-Germain kutoka kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya siku ya Jumatano, yaani wanaweza kufanya hivyo kwa uwezo wao wa ufungaji.

Uwezo wa ufungaji wa siku za jirani dhidi ya vilabu vya  Celta Vigo na Sporting Gijon umepandisha morali na imani kubwa ya mashabiki, wachezaji na makocha wa klabu hiyo wana imani kubwa kuelekea kwenye mchezo wa pili baada ya kufungwa abao 4-0 katika mchezo wa kwanza.

“Tupo katikati kwenye mchezo huu, hatuna cha kupoteza ia tutanufaika kwa ushindi na kama waliweza kufunga mabao 4, basi tunaweza kufunga mabao 6,” alisema Enrique. “Tunafika tukiwa katika kiwango bora na inabidi tujiamini katika hili.

“Bila ya kuwa na hofu, tunatakiwa kuwa na ustahimilivu na mchezo wa kwanza ilikuwa wazi kabisa tulichokifanya lakini bado ndo kwanza tupo kwenye nusu ya safari.

“Tunatakiwa kufanya mambo mengi kabisa ndani ya uwanja na kuwekeza ubora mkubwa kwenye eneo la ushambuliaji na eneo la ulinzi kwa sababu PSG ni timu ngumu na watafanya mambo yawe magumu zaidi kwa Barcelona.”

Kocha wa PSG, Unai Emery ametangaza kikosi kipana cha wachezaji waliosafiri kuelekea kwenda Barcelona lakini bado hakuweka wazi aina gani ya wachezaji atakaowachagua kucheza dhidi ya Barcelona.

“Wachezaji wowote kati ya 20 waliokuwepo naweza kuwatumia kwa pamoja kwenye mchezo huu,” alisema Unai Emery.

“Tunaweza kucheza kwa mbinu tofauti na siwezi kutoa vidokezo vyovyote kwa Unai alisema pia Enrique.

“Kila mmoja anatakiwa atimize majukumu na kufahamu kuwa michezo inaweza kukuweka katika hali yoyote ile na tofauti. Kama hii timu haikuwahi kuhitaji kurudi mchezoni kwa aina hii basi ni kwa sababu tumefanya vyema katika mechi za kwanza.”

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here