Home Kimataifa Huyu ndiye Andrea Belotti mwenye thamani ya euro milioni 100

Huyu ndiye Andrea Belotti mwenye thamani ya euro milioni 100

11805
0
SHARE

VILABU vikubwa barani ulaya vinamtolea macho mshambulizi wa Torino Andrea Belotti ambaye alifunga magoli matatu ‘Hat trick’ katika ushindi wa 3-1 ambao Torino waliupata siku ya jana Jumapili dhidi ya Palermo katika ligi kuu ya Italia ‘Serie A.’

Chelsea chini ya kocha Mtaliano, Antonio Conte, Manchester United, Arsenal, FC Bayern Munich, Borussi Dortimund ni baadhi ya timu kubwa za ulaya ambazo zinapendezwa na mshambuliaji huyo kijana aliyefunga magoli 21 msimu huu katika Serie A.

Belotti ametokea wapi

01: Alizaliwa Disemba 20, 1993 katika mji wa Caccinate, huko Italia. Ana umri wa miaka 23 hivi sasa.

02: Akiwa na miaka kumi alijiunga na timu ya vijana ya Grumellese. Kati ya mwaka 2003 hadi 2006 alidumu katika timu hiyo kisha akahamia Albino Leffe hadi mwaka 2012.

03: Alipandishwa katika kikosi cha wakubwa msimu wa 2012/13 na kufunga magoli 14 katika michezo 37 aliyoichezea AlbinoLeffe.

04: Agosti 2013 alijiunga na Palermo kwa mkataba wa mkopo akitokea Albino Leffe kabla ya kununuliwa kwa usajili wa kudumu Julai 2014.

05: Septemba 24, 2014 alifunga goli lake la kwanza katika Serie A wakati Palermo ilipotoka sare ya 3-3 dhidi ya Napoli. Belotti alifunga magoli mawili katika mchezo huo.

Alifunga jumla ya magoli 16 katika michezo 62 aliyoichezea Palermo.

07: Agosti 18, 2016 Belotti alijiunga na Torino kwa ada ya euro 7.5 milioni. Novemba 28 akafunga goli lake la kwanza katika Serie A akiichezea Torino katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Bologna.

08: Baada yb kufanya vizuri msimu huu, Disemba 4, 2016, Belotti aliongeza mkataba wa kuendelea kuichezea Torino hadi mwaka 2021 huku kukiwa na kipengele  cha kumruhusu kujiunga na timu nyingine itakayofikb na dau
lisilopungua euro milioni 100 kwa klabu za nje ya Italia.

09: Machi 5, 2017 Belotti alitumia dakika nane kufunga magoli matatu ‘ hat trick’ dhidi ya timu yake ya zamani Palermo na kufikisha magoli 20 katika Serie. Sasa anafukuzia relodi ya Benjamin Santos ambaye alifunga
magoli 27 katika msimu wa 1949/50 akiwa klabuni Torino.

10: Belotti  amezichezea timu za Taifa za vijana za Italia, alifunga magoli mawili katika michezo 6 aliyoichezea Italia U19, akafunga magoli manne katika michezo tisa aliyoichezea Italia U20, akafunga magoli 9 katika michezo 18 aliyoichezea Italia U21.

Agosti 27, 2016 aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya wakubwa ya Italia chini ya kocha Gian Piero Ventura kwa ajili ya mchezo wa kirafiki vs Ufaransa.

Alifunga goli la kwanza akiichezea Italia katika ushindi wa
3-2 ugenini dhidi ya Macedonia Oktoba 9 katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia 2018.

Hadi sasa ameichezea Azurri michezo mitano na kufunga magoli matatu.

Makala haya yameandaliwa na Baraka Mbolembole

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here