Home Kitaifa Chirwa anaamini ubingwa wa VPL unaenda Jangwani

Chirwa anaamini ubingwa wa VPL unaenda Jangwani

5088
0
SHARE

Zainabu Rajabu

STRAIKA wa Yanga Obrey Chirwa amesema bado wana nafasi ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa bado wataendelea kupambana vizuri kwenye mechi zijazo ili kupata matokeo mazuri.

Chirwa ambae kwasasa amekuwa na msaada mkubwa katika kikosi cha Kocha mkuu George Lwandamina, huku akiwa amepachika magoli nane katika ligi kuu  tangu alipo sajiliwa na  Yanga akitokea Platinum ya Zimbabwe.

Chirwa ameiambia shaffihdauda.co.tz: “Huwezi kututoa kwenye mbio za ubingwa kwa mechi mbili ambazo kwetu tumeambulia alama moja.

“Mimi bado naamini tukishikamana vizuri kuanzia viongozi hadi wachezaji nina imani kombe linabaki mitaa ya Jagwani,” alisema Chirwa.

Nyota huyo ambae  usajili wake ulizua gumzo kwa mashabiki  hadi kwa wazee wa Yanga kama (mzee Akilimali) huku wakimuona hafai amesema penati aliyokosa Msuva ilisababishwa na uwanja kuwa mbovu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here