Home Kitaifa ‘Mashabiki wamenirudisha kwenye kiwango’ – Mavugo

‘Mashabiki wamenirudisha kwenye kiwango’ – Mavugo

4596
0
SHARE

Zainabu Rajabu

MSHAMBULIAJI wa Simba Laudit Mavugo amesema kuzomewa kwake kipindi wakati hafanyi vizuri uwanjani ndiyo kumemfanya awe vizuri  kwa sasa.

Mavugo alikuwa anazomewa sana na mashabiki  wa  Simba huku wakimtolea maneno  ya kejeli pindi alivyokuwa hafungi magoli na wala hakuwa  na msaada kwa timu.

Shaffidauda.co.tz ilipiga  stori na straika huyo ambae kwasasa amekuwa lulu kwa wana Simba na amesema hizo zilikuwa changamoto kwake kutokana na kila shabiki kuwa na uchu wa kumuona anafunga magoli.

“Unajua mimi kama mchezaji nisipofanya vizuri mashabiki wana haki ya kupiga kelele kwa sababu wanaona mimi sina faida kwenye timu yao na ikiwa nimesajiliwa kwa pesa nyingi,” alisema Mavugo.

Raia huyo wa Burundi amesema, mfumo wa kocha wake Joseph Omog awali ulikuwa unampa wakati mgumu sana lakini kwa sasa nimeweza kuendana nao ndiyo maana napachika mabao.

Mavugo amepachika magoli saba hadi sasa kwenye ligi kuu tangu alivyojiunga na wekundu wa Simba msimu huu akitokea  Vital’O ya Burundi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here