Home Kitaifa Jini la Majimaji linaendelea kuitesa Mtibwa Sugar

Jini la Majimaji linaendelea kuitesa Mtibwa Sugar

4579
0
SHARE

Unaweza ukasema ni gundu, Mtibwa Sugar haijashinda mechi yoyote ya ligi kuu Tanzania bara tangu ilipoifunga Majimaji FC kwa goli 1-0 December 28, 2016 kwenye uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.

Katika mechi mechi sita ilizocheza baada ya hapo haijapata matokeo ya ushindi zaidi ya sare na vipigo iwe ni mechi za nyumbani au ugenini.

Katika mechi sita za mwisho ilizocheza, Mtibwa imetoka sare mechi nne na kupoteza mechi mbili. Huku ikiwa na kumbukumbu ya kipigo kizito cha magoli 5-0 kutoka kwa Mbao FC ambao wamepanda msimu huu kucheza ligi kuu.

Tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga, mambo hayajawa mazuri kwa kocha wa sasa Zuberi Katwila. Mayanga ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na kuwaacha mabingwa hao wa zamani wa VPL wa mwaka 1999 na 2000.

Mtibwa bado inateseka kutafuta ushindi wake wa kwanza ndani ya mwaka 2017 katika mechi za ligi kwa sababu ushindi wake wa mwisho ulikuja mwishoni mwa mwaka 2016 ilipoifunga Majimaji kwenye mchezo wa ligi.

Matokeo ya Mtibwa Sugar katika mechi sita mfululizo zilizopita za ligi kuu Tanzania bara 2016/17

28/12/2016 Mtibwa Sugar 1-0 Majimaji

18/01/2017 Mtibwa Sugar 0-0 Simba

30/01/2017 Kagera Sugar 2-1 Mtibwa Sugar

05/02/2017 Mbao FC 5-0 Mtibwa Sugar

12/02/2017 African Lyon 2-2 Mtibwa Sugar

19/02/2017 Mtibwa Sugar 0-0 JKT Ruvu

05/03/2017 Mtibwa Sugar 0-0 Yanga

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here