Home Kimataifa Antolella shemeji yetu kwa Messi ana haya mambo usiyoyajua.

Antolella shemeji yetu kwa Messi ana haya mambo usiyoyajua.

10337
0
SHARE

Cristiano Ronaldo ana gundu na wanawake,ama pengine yeye ni Play Boy.Dunia iliamini angemuoa Irina Shayk lakini huwezi amini Irina aliitosa siku ya kuzaliwa ya mama mkwe wake na kwenda batani.Upande wa Lioneil Messi amembwaga Ronaldo katika mahusiano,Messi anafurahia uhusiano wa miaka 22 na mpenzi wake Antonella.Pengine hujui mambo kadhaa kuhusu Antonella.Tulia hapo hapo na soma mambo matano usiyoyajua kuhusu shemeji yetu kwa Messi.

1.ANAPENDA HARRY PORTER,MBWA NA DISNEY.Antonella tofauti na mademu wa mastaa wengine,anapenda sana kusoma vitabu haswa Harry Porter na Cursed Child.Ana akaunti Instagram lakini Antonella hapendi sana kuonekana,mara nyingi katika akaunti yake huwa unawapost wanae wawili pamoja na baba yao.Ana mbwawake watatu hao,ukiwagusa hao huwa ni ugomvi mkubwa sana,Anapenda sana Disney na mara kadhaa amekuwa akipost picha wakiwa Desney yeye Messi.Na hata akikosa cha kupost Instagram hupost vipande vya video vya Disney.

2.NI MSIRI SANA NA HAPENDI KUONEKANA ONEKANA.Sijui hata wewe lini ulimskia Antonella akiongelewa na vyombo vya habari,sio vitu vyake hivyo kwani yeye hupenda kukaa mbali sana na waandishi wa habari.Pamoja kuwa na uhusiano wa miaka mingi na mchezaji ambae kila baada ya lisaa huezi kuacha kumuona akizungumzia lakini Antonella yeye hataki kabisa mambo hayo.Mwaka 2009 wakati Messi anauambia ulimwengu kwamba ana mpenzi waandishi wa habari walihangaika sana kumtafuta Antonella na kuongea nae lakini walishindwa.Ameshaonekana mara kadhaa akiwa na mumewe na mwanae katika utoaji wa tuzo.
3.MESSI ALITAKA KUMUOA MIAKA 20 ILIYOPITA.Antonnella alikuwa katika uhusiano na Messi tangu Messi akiwa na miaka 8 na sasa ana 28.Unaambiwa toka Lioneil akiwa katoto alikuwa anatamani tu kumuoa Antonella.Marafiki wengi wa utoto wa Messi waliamini siku moja Messi na Antonella watapata mtoto.Ndoto iliyotimia mwaka 2009 baada ya Messi kuanza rasmi uhusiano sasa wa serious kati yake na Antonella(uchumba).Baada ya kukaa kama wachumba kuanzia 2009 Lioneil Messi na Antonella wamepanga mwaka huu usiishe bila wao kufunga pingu za maisha.
4.SIO MREMBO TU,ANA AKILI BALAA.Antonella tofauti na wasichana wengine ambao difa yao ni uzuri tu.Familia yake sio nzuri sana kifedha lakini hii haikumkatisha tamaa kufikia ndoto zake,kipindi kabla hajahamia Hispania wakati Messi hajawa tajiri,Antonella alifanya kazi nyingi za kujitolea ili apate pesa akasome.Ni mtundu sana lakini pia mpole sana,marafiki zake wengi huwa wanamtegemea kiushauri na wamekuwa wakimsifu kwamba ni mrembo mwenye akili.
5.ALIMFAHAMU MESSI AKIWA MDOGO SANA.Urafiki wa Messi na Antonella ulianza wakiwa na miaka 9,lakinj walijuana kabla ya hapo.Inasemekana Antonella alimjua Messi tangu akiwa na miaka mitano tu.Kuanzia hapo wakakua pamoja na kauhusiano kakitoto toto kakaanza Messi akiwa na miaka 9 kabla ya 2009 kuanza kuwa wapenzi rasmi,tuwatakie kila la kheri wanapoelekea kufunga ndoa mbeleni mwaka huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here