Home Kitaifa Kichuya kawaliza tena Yanga

Kichuya kawaliza tena Yanga

12274
0
SHARE

Simba imepata ushindi wake wa kwanza kwenye ligi tangu March 8, 2015 ilipopata ushindi wa goli 1-0. Mechi nyingine tatu zilizofata baada ya hapo, Simba ilipoteza michezo miwili (msimu uliopita kwa kufungwa magoli 2-0) halafu wakatoka sare ya kufungana goli 1-1 msimu huu kwenye raundi ya kwnza.

Mchezo wa leo  ulikuwa ni muhimu kwa timu zote mbili kwa sababu timu zote ziko kwenye mbio za ubingwa wa msimu huu.

Yanga walianza kupata goli dakika ya tano ya mchezo kwa mkwaju wa penati baada ya Novalty Lufunga kumwangusha mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa kwenye eneo la hatari wakati akielekea kufunga.

Simon Msuva akakwamisha kambani mkwaju huo kwa kupiga mpira upande wa kushoto wa golikipa Daniel Agyei lakini ukiwa ni upande wa kulia wa Msuva.

Baada Simba kuruhusu goli, kocha wa Simba Joseph Omog alifanya mabadiliko kwa kumtoa Juma Liuzio na kumuingiza Said Ndemla ambaye kwa kiasi kikubwa akaituliaza timu kwenye nafasi ya kiungo wa kushambulia.

Kipindi cha kwanza kikamalizika Simba wakiwa nyuma kwa goli moja huku Yanga wakiwa mbele kwa goli moja la Simon Msuva.

Kipindi cha pili wakati Simba ikiwa inapambana kupata goli la kusawazisha, ikpata pigo baada ya beki wao wa kulia Javier Bokungu kuondolewa uwanjani kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Obrey Chirwa nje kidogo ya eneo la box.

Kocha wa Simba akafanya tena mabadiliko kwa kumuingiza Shiza kichuya kuchukua nafasi ya Mohamed Ibrahim ‘MO’.

Kadi nyekundu ya Bokungu ikalazimisha benchi la ufundi la Simba kufanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Novalty Lufunga kisha akaingia Jonas Mkude ambaye alienda kucheza nafasi ya kiungo wa ulinzi aliyokuwa ikichezwa na James Kotei ambaye alirudi kucheza katika beki ya kati sambamba na Abdi Banda.

Simba wakapata bao la kwanza na la kusawazisha dakika ya 66 lililofungwa na Laudit Mavugo kwa kichwa aliyeunganisha pasi ya Kichuya kutoka upande wa Kaskazini Mashariki ya uwanja.

Kichuya akapeleka ushindi Msimbazi baada ya kufunga bao la pili huku likiwa ni goli lake la 10 msimu huu katika ligi kuu Tanzania bara.

Simba bado wanaongoza ligi wakiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 23 huku Yanga wakisaliwa na pointi zao 49 pointi tano nyuma ya Simba lakini Yanga wanamchezo mmoja mkononi wakiwa wamecheza mechi 22.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here