Home Kimataifa “Wapige United beba kombe tukuheshimu” kocha wa Southampton kaambiwa

“Wapige United beba kombe tukuheshimu” kocha wa Southampton kaambiwa

5279
0
SHARE

Kocha wa zamani wa timu za Southampton Lawrie McMenemy amemuandikia barua kocha wa timu hiyo wa sasa Claude Puel.Barua ya Lawrie kwa Claude inamsisitiza Claude kuhusu umuhimu wa kuifunga Manchester United siku ya Jumamosi katika fainali ya kombe la EFL.

McMenemy ambae anatajwa kati ya makocha waliowahi kuwa na mafanikio Southampton amemwambia Claude kwamba kama anahitaji kuweka historia muhimu klabuni hapo baasi hio ndio nafasi yake.Mwaka 1976 McMenemy aliingia kwenye vitabu vya historia ya Southampton baada ya kuifunga United katika fainali ya FA.Kama hiyo haitoshi mwaka 1979 tena McMenemy aliifikisha Southampton fainali ya kombe la ligi lakini walipoteza mchezo huo dhidi ya Nottingham Forest.
“Sijawahi kuonana na Claude,lakini mwezi uliopita baada ya kuwafunga Liverpool nilikwenda ofisini kwake nikamuachia barua,nimemtakia kila la kheria na naamini atafanya zaidi ya kile nilichofanya 1979 baada ya kupoteza katika fainali ya mashindano haya wakati huu unaweza kuwa wetu” alisema McMenemy.
Toka Southampton wachukue kombe la FA mwaka 1976 hawajawahi kuchukua tena kombe lolote na McMenemy analiona hilo kama tatizo kwao na kumkumbushia Claude kuhusu ukame huo.Lakini McMenemy akiiangalia Southampton anakosa uhakika kama kweli wanaweza kuizuia Manchester United haswa katika eneo lao la beki.
Beki ya Southampton kwa misimu kadhaa imekuwa chini ya uangalizi wa mlinzi wa Kireno Fonte ambae sasa amehamia Westham.McMenemy anaamini Virgil Van Djik ndio mlinzi bora kwa sasa katika ligi kuu ya Uingereza.”Kila nikimtazama Djik anazidi kuimarika na sasa ni mlinzi bora hapa Uingereza,akicheza na Fonte walikuwa bora sana lakini ni aibu Fonte kaondoka”.
Wakati Fonte ameondoka Southampton,mlinzi anayetajwa bora na McMenemy Van Djik naye ni majeruhi na hana uhakika kucheza siku ya Jumamosi.Huku United nao wakiwa hatiani kumkosa Mkhitaryan na Michael Carrick kutokana na majeruhi waliyoyapata katika mchezo dhidi ya St Ettiene.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here