Home Ligi EPL Dembele wa Dortmund Aongoza Wachezaji bora 30 Vijana, Rashford yumo.

Dembele wa Dortmund Aongoza Wachezaji bora 30 Vijana, Rashford yumo.

4678
0
SHARE

Inawezekana mpaka sasa ukawa unajiuliza wachezaji gani vijana ni bora mpaka sasa. Inawezekana jina la Marcus Rashford likawa linakuja haraka kichwani kwako, au pengine Davies wa Everton kwa wale wanaopenda ligi kuu ya Uingereza lakini ambo yapo tofauti kidogo.

Jarida la nchini Italia, Gazzetta dello Sport limemtaja mchezaji wa  Manchester United kinda Marcus Rashford kuwa mchezaji wa 4 kwa ubora kati ya vijana 30 bora barani Ulaya huku kutoka Uingereza vijana kutoka Fulham na Everton wakiingia kwenye orodha.

Mchezaji bora kinda na namba moja kwa Ulaya ametajwa Ousmane Dembele kutoka katika klabu ya Borussia Dortmund, na raia wa Ufaransa huku kinda na golikipa wa klabu ya AC Milan, Gianluigi Donnarumma  mwenye umri wa miaka 17 akiwa katika nafasi ya 2.

Kiungo Renato Sanches wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ureno, yupo katika nafasi ya 3 na ya nne imekwenda kwa Rashford. Nafasi ya 5 ni mchezaji wa klabu ya Monaco, night Kylian Mbappe ambaye aliwafunga Manchester City siku ya Jumanne na nafasi ya sita yupo kiungo Ruben Neves ambaye aliweka rekodi ya kuwa nahodha mdogo zaidi kwenye historia ya UEFA mwaka jana.

Ousmane Dembele is regarded as the most exciting prospect in Europe

Kumi bora inakamilishwa na wachezaji Malang Sarr, Kasper Dolberg, Breel Embolo na Mikel Oyarzabal.

Kinda anayekuja kwa kasi nchini Uingereza Sessegnon  na kiungo wa Everton Davies wametajwa kwenye nafasi ya 26 na 28 huku mchezaji aliyevuta hisia za watu wengi na sakata lake la usajili kabla hajasajiliwa na Real Madrid,  Martin Odegaard akiwa katika nafasi ya 29.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here