Home Kitaifa Maandalizi ya kipekee kuelekea Simba na Yanga, Vipi makocha kupangiwa timu? Chuji...

Maandalizi ya kipekee kuelekea Simba na Yanga, Vipi makocha kupangiwa timu? Chuji kafunguka

7195
0
SHARE
Chuji akijifua uwanjani Mwadui Complex, Shinyanga

Tumezoea kuona kila inapokaribia mechi ya Simba na Yanga timu hizi zinapewa muda mrefu wa kujiandaa na mechi husika tofauti na pale zinapokuwa zinacheza na timu nyingine za ligi. Mara nyingi timu hizi zimekuwa zikifanya maandalizi yao nje ya Dar, kwa mfano kuelekea mechi ya February 25 tayari Simba wapo Zanzibar huku Yanga wao wakiwa Kigamboni wakiendelea na mazoezi.

Athumani Idd ‘Chuji’ amewahi kucheza kwenye timu hizi mbili kwa nyakati tofauti, kuelekea mechi ya watani wa jadi amezungumzia maandalizi yanayofanyika lakini akasema hakuna kitu cha kipekee kinachofanywa tofauti na mechi nyingine zaidi ya hamasa kwa wachezaji.

Lakini pia akazungumzia kuhusu makocha kupangiwa wachezaji wa kucheza siku ya mchezo wa mechi ya Simba na Yanga, kila kiongozi au matajari wanapanga vikosi vyao na kumkabidhi mwalimu nani acheze na yupi asicheze.

“Ikishafikia mechi ya Simba na Yanga hakuna kitu kipya kinachofanyika zaidi ya hamasa, ni matajiri tu wanapishana kambini, leo anakuja huyu kesho atakuja yule wote wanakuja na ahadi zao lakini maandalizi ya maana hakuna.”

“Ambaye alikuwa anaweza kuiandaa timu ni kocha mmoja tu, James Siang’a lakini hawa makocha wote wanaokuja hakuna kazi wanayofanya ikifika Simba vs Yanga. Nikisema kuna maandalizi ya maana ntakuwa nawaongopea watanzania.”

“Ikikaribia mechi ya Simba na Yanga unaweza kukuta kuna line up zaidi ya saba, matajiri wanakuja kambini na vikosi vyao, kila mmoja anataka watu wake wacheze, huyu anampanga flani akija mwingine hamtaki. Kwa hiyo matajiri kwa kiasi kikubwa wanawapangia waalimu vikosi wanavyovitaka wao na sio vikosi kupangwa na makocha.”

“Makocha ambao walikuwa na maamuzi magumu ni Jack Chamangwana, Micho na Siang’a ndio makocha pekee ambao walikuwa wanaweza kusimamia maamuzi yao na walikuwa na maamuzi magumu.”

Siang’a aliondoka Simba kwa sababu alipunguzwa na viongozi wakiwa na sababu zao binafsi, baada ya kupata mafanikio kuna viongozi wakawa wanataka waingilie kazi yake ili waonekane wao ndio wanaleta mafanikio hayo. Yule mzee alikataa kufanya mambo kwa maagizo ya viongozi na hapo ndipo akajikuta anapunguzwa na viongozi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here