Home Kimataifa Chama Cha Soka Nigeria, Kimemtosa Issa Hayatou.

Chama Cha Soka Nigeria, Kimemtosa Issa Hayatou.

2189
0
SHARE
ZURICH, SWITZERLAND - OCTOBER 13: FIFA Senior Vice President Issa Hayatou sits in the lobby during part I of the FIFA Council Meeting 2016 at the FIFA headquarters on October 13, 2016 in Zurich, Switzerland. (Photo by Philipp Schmidli/Getty Images)

Shirikisho la soka nchini Nigeria NFF linamuunga mkono Rais wa chama cha soka nchini Madagascar Ahamad Ahmad katika uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Rais wa NFF Amanju Pinnick amesema CAF inahitaji kizazi kipya cha uongozi ambacho kitaweza kwenda sawa na kasi ya uongozi mpya wa FIFA .

Pinnick ameongeza kuwa pamoja na kwamba rais wa sasa Issa hayatou ana nafasi kubwa ya kushinda yeye anaamini jukumu hilo ni zito kwa ukongwe wa Issa na Vijana kama Ahmad wanapaswa kupewa nafasi.

“Tumeamua kumsapoti Ahmad kwa sababu ni mtu jasiri aliyejitokeza kupambana na mkongwe Hayatou aliyeongoza CAF  kwa vipindi vinane”

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here