Home Kitaifa Busungu anataka kufata nyayo za Nonga kuachana na Yanga

Busungu anataka kufata nyayo za Nonga kuachana na Yanga

7937
0
SHARE
Malimi Busungu mshambuliaji wa Yanga aliyefunga goli la pili wakati timu yake ikicheza na Simba na kutengeneza goli lililofungwa na Amis Tambwe

Na Zainabu Rajabu

Mshambuliaji wa Yanga Malimi Busungu amesema anataka kuachana na klabu hiyo baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha mzambia George Lwandamina.

Mshambuliaji huyo ambae alikuwa na msaada mkubwa katika msimu uliopita na kuisaidia timu yake kunyakua ubingwa wa ligi pamoja na FA Cup amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha Yanga chini ya Lwandamina huku mwalimu huyo akipendelea kuwatumia Amis Tambwe pamoja Donald Ngoma katika safu ya ushambuliaji.

Busungu ameiambia shaffihdauda.co.tz kuwa anasubiri msimu huu umalizike ili aone kama ataweza kujiunga na timu ambazo zinahitaji huduma yake.

“Nasubiri msimu huu uishe kwasababu tayari kuna baadhi ya timu za ligi kuu zinataka huduma yangu licha ya mkataba wangu na Yanga kubaki miezi sita.”

“Timu nyingi zinanitaka ila nimeandika barua katika uongozi wa Yanga kuniruhusu kuondoka, licha ya kubakiza mkataba wa miezi sita kuitumikia klabu hiyo ambayo nimekuwa sina nafasi katika kikosi hicho.”

Ni muda mrefu sasa umepita bila busungu kuonekana kwenye kikosi cha Yanga hata kwenye mazoezi ya kikosi cha timu hiyo amekuwa haonekani pia, lakini uongozi wa timu hiyo mara zote umekua ukisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Mgambo JKT anaandamwa na matatizo ya kifamilia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here