Home Kimataifa Mtihani Usiozungumzwa Kwa Man City. Wanaitwa Monaco.

Mtihani Usiozungumzwa Kwa Man City. Wanaitwa Monaco.

4697
0
SHARE

Kocha wa klabu ya Monaco, Leonardo Jardim amefanikiwa kutengeneza kikosi chenye damu changa na ambacho kinategemewa kuwastua wengi msimu huu. Katika kikosi hicho ni Falcao, beki Kamil Glik na kipa Daniel Subasic pekee ambao wenye umri wa miaka 26 au zaidi.

Hiki ni kikosi ambacho wakati kinapangwa na Manchester City wengi wangeweza kufikiri kuwa ilikuwa ni utelezi tu kwenda kwenye raundi nyingine kwa uande wa Man City. Lakini ukiachana na uzito wa vikosi kwenye karatasi, Monaco wanaweza kuzua baya lolote ambalo halikutegemewa.

Lakini ulikuwa ufahamu, Monaco wanafika kwenye uwanja wa Etihad siku ya Jumanne kama kikosi chenye safu ya ushambuliaji hatari zaidi barani Ulaya kwa sasa, wakiwa ni vijana wadogo, wenye kasi na nguvu na ambao hawaogopi kufika kwenye goli la wapinzani. Na pale unapowaza safu ya Ulinzi ya Man City lazima ushike tama.

Monaco are heading to Manchester City on Tuesday night for their last-16 encounter

Mpaka sasa, Man City ndiyo inayotegemewa zaidi kwa Uingereza kama mwakilishi mwenye nafasi kubwa zaidi ya kufika katika hatua ya robo fainali, lakini tofauti na wengi wanavyodhani, watakutana na klabu ambayo imefunga mabao 107 kwenye michuano yote mpaka sasa.

Paris Saint-Germain, ambao wanaogopeka na ambao wameweza kuonyesha ubabe wao kwa Barcelona kwenye mchezo uliopita hawajawa karibu kwa Monaco msimu huu. Hawa wamefanya kila kilichokuwa bora.

Monaco inayoongozwa na Falcao, ina damu changa kama Tiemoue Bakayoko, mchezaji muhimu mwenye nguvu kwenye eneo la kiungo, winga Bernardo Silva, mshambuliaji Kylian Mbappe na Lemar. Wamekomaa katika umri mdogo sana.

Monaco have scored 107 goals in all competitions this term - more than anyone in Europe

Huu unaweza kuwa mtihani mkubwa sana kwa Guardiola tofauti na watu wengi wanavyoweza kufikiri. Hii timu ina nguvu, eneo la kiungo Bakayoko na Fabinho wamekuwa  na muunganiko mzuri na si ajabu kuona wakiwindwa na vilabu vikubwa kila kukicha. Lakini hata mawinga wao wanapata huduma nzuri kutoka pembeni kwa mabeki kama Benjamin Mendy ambaye amekuwa na msimu bora. Kipindi kigumu kwa Man City kuliko wengi wanavyodhani hiki.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here