Home Kimataifa Jarrius Robertson.. Furaha Machoni, Huzuni Moyoni.

Jarrius Robertson.. Furaha Machoni, Huzuni Moyoni.

10673
0
SHARE
NEW ORLEANS, LA - FEBRUARY 17: New Orleans Saints Super Fan Jarrius "Little JJ" Robertson celebreates after scoring during the NBA All-Star Celebrity Game at the Mercedes-Benz Superdome on February 17, 2017 in New Orleans, Louisiana. NOTE TO USER: User expressly acknowledges and agrees that, by downloading and or using this photograph, User is consenting to the terms and conditions of the Getty Images License Agreement. (Photo by Jonathan Bachman/Getty Images) ORG XMIT: 700002606 ORIG FILE ID: 642459960

Kama uliruhusu jicho lako lifunguke, litizame michezo yote ya All Star basi ungeweza kuona kijana mdogo, mfui na machachari. Kijana ambaye huwezi kufikiri kuwa anaishi katika matumaini ingawa hafahamu ni lini nuru haitopenyeza macho yake yanayobeba uchangamfu wake.

Katika robo ya nne ya mchezo wa mastaa wa Marekani yaani NBA Celebrity game, kijana mmoja akiwa anabishana na Draymond Green alikuwa akiingia uwanjani. Ukumbi mzima ulinyanyuka pale alipopata mtupo wake. Lakini kinachowafurahisha zaidi watu sio michezo yake mtoto huyu bali ni ugumu wa maisha aliokulia na namna ambayo anajaribu kufikisha ujumbe wa kupigania maisha kwa jamii.

Jarrius Robertson ana muonekano wa mtoto wa miaka isiyozidi 10, pengine 8 kama wengi wanavyomwona lakini ana miaka 14 katika maisha ya kweli. Kijana huyu anasumbuliwa na tatizo la ini ambalo limefanyiwa pandikizi tangu akiwa na umri wa miaka 2, hali iliyomfanya kupooza kwa takribani mwaka mmoja.

Jarrius ana kauli mbiu ya maisha ndiyo yanayoweza kuokoa maisha kaiamini katika kujitolea damu, viungo kama figo na vitu vingine vya msingi kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine kama namna ambayo inaokoa maisha ya wengi hasa kwa magonjwa yasiyokuwa na tiba.

Huyu tayari ni mwanachama wa heshima wa klabu anayoishabikia ya New Orleans Saints inayoshiriki ligi ya American Football na ambayo amekuwa akihudhuria michezo yake mingi huku pia akijenga uhusiano wa karibu na wachezaji wengi wa kikosi hicho.

Kama hiyo haitoshi, kampuni inayosimamia mchezo wa mieleka Marekani, WWE ilimtumia kama balozi kwenye uzinduzi wa shindano lao maarufu zaidi yaani Wrestlemania ambapo alipata nafasi ya kuketi na mastaa kadhaa huku pia akipewa muda wa kuwahoji na kubadilishana nao mawazo.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here