Home Kimataifa Balotelli amepata kadi nyingi nyekundu kuliko magoli yake ya ugenini.

Balotelli amepata kadi nyingi nyekundu kuliko magoli yake ya ugenini.

2321
0
SHARE

Waswahili wanasema sikio la kufa halisikii dawa,sasa Mario Baloteli ni sikio la kufa.Wakati akiwa na kocha Roberto Mancini Balloteli hakuwa anaishiwa visa na kero,baadae alipoenda Liverpool hakuwa sana na matukio kwa kuwa hakupewa nafasi sasa yuko Nice na utukutu wake kama kawaida.

Wakati kapteni wa Bayern Munich Philip Lahm ikisemekana anatarajia kustaafu,amecheza mechi zaidi ya 338 tena katika nafasi ya ukabaji bila kadi nyekundu.Lakini jana Balloteli wakiwa katikati ya msimu huku akiwa amecheza msimu huu mechi zisizofika hata 20 lakini amepata kadi yake nyekundu ya tatu.
Japokuwa timu yake ya Nice iliibuka na ushindi wa goli moja dhidi ya vibonde wa ligi ya Ufaransa timu ya Lorient,Balotelli alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 68 baada ya ugomvi wake na beki wa Lorient aitwaye Zargo Toure.Baloteli alicheza mechi dhidi ya Lorient baada ya kukosa mchezo uliopita kutokana na kuugua.
Balloteli amefunga magoli tisa katika ligi ya Ufaransa huku magoli yote akiwa amefunga katika uwanja wao wa nyumbani,huku akiwa hajafunga hata goli moja ugenini.Picha za video hazioneshi wazi wazi ni nini Balloteli alikifanya,japokuwa walikuwa wanaonekana kama wanagombania mpira huku Balloteli mikono yake ikionekana kutomgusa Toure.
Inaonekana Balloteli pengine alimtolea maneno machafu Tonny Charpon ambae alikuwa muamuzi wa mchezo huo.Kocha wa Nice Lucien Favre amesema baada ya mchezo huo kwamba hadi sasa haelewi kwanini refa alimtoa Balloteli ila aliona tu kadi nyekundu ikinyanyuliwa juu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here