Home Kimataifa Baada ya miaka 103 Lincolin City yavunja rekodi ya QPR

Baada ya miaka 103 Lincolin City yavunja rekodi ya QPR

3206
0
SHARE

Ilikuwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa vita ya kwanza ya dunia mwaka 1914.Katika miaka hii timu ya Queen Park Rangers walifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Fa miaka hiyo na huo ukawa mwisho wa timu za chini kucheza robo fainali ya Fa nchini Uingereza.Robo fainali hiyo ilikuwa mwisho wao baada ya kufungwa goli 2 kwa 1 na Liverpool.

Miaka 103 sasa imepita na jana baada ya ushindi dhidi ya Burnley timu ya Lincolin City wamefanikiwa kufanya kile kilichofanywa na Queen Park Rangers miaka 103 iliyopita.Ni jambo kubwa sana kwao na katika historia ya klabu yao haswa kutokana na heshima ya Waingereza kwa michuano hiyo.
Kocha wa timu hiyo Danny Cowley amejinasibu kwamba walistahili kupata mafanikio hayo.Cowley anasema ukiangalia walivyocheza dhidi ya Burnley walipoteza 60% ya nafasi walizozipata.Cowley anaamini Burnley walipaswa kufungwa goli nyingi zaidi.
“Inabidi tujiamini,inabidi tupambane,tunaweza kuwa na nafasi.Kufika hapa ni kama kufanikiwa jambo lisilotarajiwa na tunatazamia kufanya hivyo tena” aliongeza Cowley.Goli la kichwa la Sean Raggets ndilo lililowavusha Lincolini kwenda katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Lincolini City wameingia katika vitabu vya historia ya FA kwani ndio timu ya tatu kutoka ligi daraja la pili kufuzu kwa hatua ya tano ya michuano hiyo,hapo kabla mwaka 2011 Crawley walifanya hivyo na mwaka 2013 Lutton walifanya hivyo.Lakini wanakuwa timu ya pili kutoka ligi daraja la pili kufudhu kwenda robo fainali baada ya Qpr.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here