Home Dauda TV VIDEO: Zlatan Ibrahimovic ameigawa familia ya Pogba

VIDEO: Zlatan Ibrahimovic ameigawa familia ya Pogba

17441
0
SHARE

Hat-trick ya Zlatan Ibrahimovic imeipa ushindi Manchester United wa magoli 3-0 dhidi ya Saint-Etienne kwenye mchezo wa Europa League hatua ya 32 bora uliochezwa usiku wa February 16, 2017 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mbali na ushindi wa United, mchezo ulikuwa unawakutanisha ndugu wa damu kutoka familia ya Pogba hawa ni Paul na Florentin Pogba lakini wakiwa katika timu tofauti.

Hitokei mara nyingi kwenye professional football, lakini wachezaji hawa wa familia moja ni miongoni mwa ndugu wachache waliowahi kukutana kwenye mechi dhidi ya timu zao katika ngazi ya vilabu.

Kbla ya game hiyo, kocha wa Manchester United Jose Mourinho alisema, anajua mama yao kina Pogba anaomba mchezo huo umalizike kwa sare. Mourinho alisema hivyo kwa sababu anajua sare pekee ndiyo yalikuwa matokeo ambayo yatamuacha mama yao na furaha.

Mwisho wa siku Ibrahimovic akapeleka kilio kwa Saint-Etienne na kumuacha Florentin na majonzi wakati kwa upande wa Paul yeye ni shangwe. ushindi huo unamgawa mama yao upande mmoja anafuraha kwa sababu timu ya Paul imeshinda lakini upande mwingine kwa Florentin anahuzunika kwa mwanae kufungwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here